Lugha Nyingine
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon washambuliwa na Israel
Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini Lebanon kimetoa taarifa jana tarehe 26 ilisema droni ya jeshi la ulinzi la Israel imetuma bomu dhidi ya kikosi hicho kilichokuwa kikitekeleza majukumu nchini humo na baadaye kifaru cha Israel kilifyatua risasi dhidi ya walinda amani. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mashambulizi hayo yalitokea katika saa kumi na mbili kasorobo alasiri tarehe 26 katika kijiji kimoja katika eneo la mpakani kusini mwa Lebanon, kwa bahati hakuna vifo, majeruhi au hasara ya mali iliyotokea katika tukio hilo.
Taarifa hiyo pia imelaani kuwa vitendo vya jeshi la Israel limekiuka azimio namba 1701 la Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa na kukiuka mamlaka ya Lebanon, pia imeonyesha mtazamo wake wa kupuuza usalama wa wanajeshi wa kulinda amani.
Hii ni mara ya tatu ndani ya mwezi huu kwa Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon kutoa taarifa kulaani jeshi la Israel kwa kitendo chake cha kushambulia walinzi wa amani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



