Lugha Nyingine
China na Marekani zafanya majadiliano kuhusu uchumi na biashara huko Kuala Lumpur, Malaysia

Kabla ya majadiliano ya tarehe 25, Oktoba kwa saa za Kuala Lumpur, He Lifeng, ambaye ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na naibu waziri mkuu wa serikali ya China, alipiga picha pamoja na Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent. (Xinhua/Bai Xueqi)
Kuanzia tarehe 25 hadi 26 Oktoba kwa saa za Kuala Lumpur, mwakilishi wa upande wa China kuhusu mambo ya uchumi na biashara na Marekani He Lifeng, ambaye pia ni naibu waziri mkuu wa serikali ya China, pamoja na mwakilishi wa upande wa Marekani Scott Bessent, Waziri wa Fedha, walifanya majadiliano kuhusu uchumi na biashara kati ya nchi hizo mbili huko Kuala Lumpur, Malaysia.
Pande zote mbili za majadiliano zilikuwa zikifuata maoni muhimu ya pamoja yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili katika mazungumzo yao kwa njia ya simu tokea mwaka huu, zilibadilishana maoni na kushauriana kwa udhati, kina na yenye maana ya kiujenzi juu ya hatua za Marekani zinazohusiana na Kifungu cha 301 za kulenga usafirishaji wa njia ya bahari na sekta ya uundaji wa meli ya China, kuongeza siku za kusitisha kwa muda kodi ya kulipiza kisasi, ushuru wa fentanyl na ushirikiano wa utekelezaji wa sheria, biashara ya mazao ya kilimo, usimamizi na udhibiti wa uuzaji wa nje wa nchi na masuala mengine muhimu yanayofuatiliwa nao, ambapo zimefikia maoni ya pamoja ya kimsingi juu ya mpango wa kutatua masuala yanayofuatiliwa na kila upande. Pande hizo mbili zilikubaliana kuthibitisha zaidi hali halisi ya mambo yote na kutekeleza utaratibu wa kupitisha wa kila nchi ya pande hizi mbili.
He Lifeng alisema, hali asili ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani ni kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja, na nchi hizo mbili zikishirikiana zitanufaishana, na zikipambana kila upande utapata madhara. He alisema, kulinda maendeleo ya utulivu ya uhusiano huo wa China na Marekani, kunaendana na maslahi ya kimsingi ya nchi hizo mbili na watu wao, na pia kunaendana na matarajio ya jumuiya ya kimataifa.
Upande wa Marekani ulisema, uhusiano huo wa kiuchumi na kibiashara kati ya Marekani na China ni uhusiano wa pande mbili wenye ushawishi mkubwa zaidi duniani. Upande wa Marekani ungependa kutatua migongano na kuimarisha ushirikiano na China kwa kupitia njia yenye usawa na ya kuheshimiana, na kutimiza maendeleo kwa pamoja.
Pande hizo zimekubaliana kwamba chini ya uelekezaji wa mikakati ya viongozi wa nchi hizo mbili, zitaufanya mfumo wa majadiliano ya China na Marekani kuhusu uchumi na biashara ufanye kazi yake vya kutosha, ili pande hizo mbili kudumisha mawasiliano ya karibu kuhusu ufuatiliaji wa kila upande katika sekta za uchumi na biashara, kuhimiza uhusiano wao wa kiuchumi na kibiashara kuendelea vizuri kwa utulivu na kupata maendeleo endelevu, ili kunufaisha watu wa nchi hizo mbili na kuhimiza ustawi wa Dunia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



