Lugha Nyingine
Cote d'Ivoire yafanya uchaguzi wa rais kwa utulivu huku kukiwa na mvutano wa kisiasa

(Picha/Xinhua)
Upigaji kura wa uchaguzi wa rais nchini Cote d'Ivoire ulifanyika kwa utulivu Jumamosi, ingawa idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura ilitofautiana katika vituo vya kupigia kura huko Abidjan.
Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa nchi hiyo, Vagondo Diomande amesema, vituo vyote vya kupigia kura vilifunguliwa na kufanya kazi, na vikosi vya usalama vilivyowekwa kwa wiki tatu, vinatimiza kikamilifu majukumu yao.
Habari zinasema, jumla ya askari polisi 44,000, mgambo na wanajeshi walikusanywa kote nchini kulinda usalama wakati wa upiga kura.
Uchaguzi huo umefanyika katika mazingira yenye mvutano wa kisiasa kufuatia mahakama kuwazuia viongozi wawili wakuu wa upinzani, Laurent Gbagbo na Tidjane Thiam kugombea katika uchaguzi huo.

Rais wa Cote d'Ivoire akipiga kura kwenye kituo mjini Abidjan wakati wa uchaguzi mkuu wa Cote d'Ivoire wa mwaka 2025. (Xinhua/Zhang Jian)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



