Lugha Nyingine
Zimbabwe yatoa wito wa kuondolewa bila masharti kwa vikwazo vya nchi za Magharibi

Vijana wa Zimbabwe wakishika bango la kupinga vikwazo vya nchi za Magharibi mjini Harare, Zimbabwe, Oktoba 25, 2025. (Xinhua/Tafara Mugwara)
Wananchi wa Zimbabwe jumamosi wameadhimisha Siku ya Kupinga Vikwazo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Harare, wakitoa wito wa kuondolewa bila masharti kwa vikwazo vilivyowekwa na nchi za Magharibi dhidi ya nchi yao miongo miwili iliyopita.
Siku ya Kupinga Vikwazo inayoadhimishwa Oktoba 25, ilianzishwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) mwaka 2019, kama pendekezo la jumla la kanda hiyo kupinga vikwazo vilivyowekwa nchini Zimbabwe kufuatia mradi wa mageuzi ya ardhi ambao uligawa upya ardhi kutoka kwa wakulima wachache weupe na kuwapa wazawa wa Zimbabwe.
Akihutubia katika maadhimisho ya siku hiyo, rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amesema licha ya changamoto zinazotokana na vikwazo hivyo, Zimbabwe inaendelea kushikilia ushirikiano wa kimataifa na wa pande nyingi kuelekea kutimiza amani, usalama, haki na maendeleo yenye usawa duniani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



