Li asema China iko tayari kusukuma mbele Pendekezo la Usimamizi wa Dunia kwa ajili ya amani na maendeleo ya kikanda

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 28, 2025

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria Mkutano wa 20 wa Viongozi wa Asia Mashariki mjini Kuala Lumpur, Malaysia, Oktoba 27, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria Mkutano wa 20 wa Viongozi wa Asia Mashariki mjini Kuala Lumpur, Malaysia, Oktoba 27, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

KUALA LUMPUR - Waziri Mkuu wa China Li Qiang jana Jumatatu alipokuwa akihutubia Mkutano wa 20 wa Viongozi wa Asia Mashariki (EAS) uliofanyika nchini Malaysia amesema kuwa China iko tayari kujumuika na pande mbalimbali katika kusukuma mbele kwa nguvu zote Pendekezo la Usimamizi wa Dunia, na kufanya juhudi za pamoja kuingiza nishati chanya zaidi katika amani na maendeleo ya kikanda.

Li amesema kuwa miaka 20 iliyopita, EAS ilianzishwa rasmi Kuala Lumpur, na katika miongo miwili iliyopita, mkutano huo umekuwa ukitekeleza jukumu la kiujenzi kwa ujumla, kuhimiza utulivu na maendeleo ya haraka katika kanda.

"Leo, dunia imeingia katika kipindi kipya cha misukosuko na mabadiliko, huku amani na maendeleo vikikabiliwa na hatari na changamoto nyingi mpya," Li amesema.

Amebainisha kuwa, Rais wa China Xi Jinping akiwa na msimamo wa kushughulikia mabadiliko hayo duniani na kukabiliana na mambo magumu, kwa dhati alitoa Pendekezo la Utawala wa Dunia.

"Likisisitiza kutilia maanani usawa wa uhuru, kufuata utawala wa sheria wa kimataifa, kutekeleza mfumo wa pande nyingi, kutetea mbinu inayoweka watu katika kipaumbele cha juu, na kujikita katika kuchukua hatua halisi, pendekezo hili linahusiana sana na masuala yaliyopo na linaendana kwa karibu na madhumuni ya kuanzishwa EAS," Li ameongeza.

China iko tayari kushirikiana na pande zote ili kuendelea kuwa mwaminifu kwa matarajio ya awali ya EAS, Li amesema, akitoa wito kwa pande zote kuendelea kujenga maafikiano mapana.

"Kuheshimiana, usawa, na kutendeana kwa haki na usawa, pamoja na mengine, ni misingi muhimu inayosimamia uhusiano kati ya mataifa. Utandawazi wa kiuchumi na dunia yenye ncha nyingi haviwezi kurudishwa nyuma, na dunia haipaswi kurudi kwenye sheria ya mwituni ambapo pande dhaifu huanguka kwa wenye nguvu," amesema.

Li amebainisha hitaji la kujikita katika kutatua matatizo makubwa, akisema kwamba maendeleo ya kiuchumi na uboreshaji wa maisha ya watu vinabaki kuwa vipaumbele vya juu kwa nchi katika kanda hiyo.

Ametoa wito wa dhamira kubwa zaidi katika kushikilia mfumo wa biashara huria, kufanya juhudi za kujenga mtandao wa biashara huria wa kikanda wa ngazi ya juu, na kwa nguvu zote kusukuma mbele mafungamano ya kikanda.

Mkutano huo, ulioongozwa na Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim, umepitisha Azimio la Kuala Lumpur katika Maadhimisho ya Miaka 20 tangu kuanzishwa EAS, na Taarifa ya Viongozi kuhusu Kuhimiza Ujanibishaji katika Hatua za Mapema za Kujiandaa Tayari na Kukabiliana na Maafa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha