Rais wa Malawi atoa amri tendaji inayopiga marufuku usafirishaji kuuza nje madini ghafi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 28, 2025

Picha hii iliyopigwa Septemba 18, 2025 ikionyesha Mnara wa Ukumbusho wa Vita na sanamu ya Hastings Kamuzu Banda, mjini Lilongwe, Malawi. (Xinhua/Peng Lijun)

Picha hii iliyopigwa Septemba 18, 2025 ikionyesha Mnara wa Ukumbusho wa Vita na sanamu ya Hastings Kamuzu Banda, mjini Lilongwe, Malawi. (Xinhua/Peng Lijun)

LILONGWE - Rais wa Malawi Peter Mutharika ametoa amri tendaji inayopiga marufuku usafirishaji kuuza nje madini ghafi, ambayo hayajachakatwa wakati nchi hiyo ikijiandaa kuendeleza rasilimali zake mbalimbali za madini.

Amri hiyo iliyotolewa Jumamosi, inathibitisha tena dhamira ya serikali ya "kuhakikisha maendeleo na matumizi endelevu ya rasilimali za madini, na kuhimiza ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia kuongeza thamani na maendeleo ya viwanda."

Rais huyo amesema madhumuni ya amri hiyo ni kupiga marufuku usafirishaji kuuza nje wa madini ghafi, kufanya kazi ya utengenezaji wa bidhaa zenye thamani ya nyongeza ndani ya nchi, na kuhakikisha kwamba maliasili za madini za nchi hiyo zinachangia kwenye maendeleo ya uchumi na ustawi wa nchi.

Kwa mujibu wa amri hiyo tendaji, marufuku hiyo ilianza kutumika rasmi Oktoba 21, 2025.

Picha hii iliyopigwa Septemba 19, 2025 ikionyesha mwonekano wa mji wa Lilongwe, Malawi. (Xinhua/Peng Lijun)

Picha hii iliyopigwa Septemba 19, 2025 ikionyesha mwonekano wa mji wa Lilongwe, Malawi. (Xinhua/Peng Lijun)

"Usafirishaji huu wa kuuza nje madini ghafi kutoka Malawi umepigwa marufuku. Marufuku hii itatumika kwa madini yote yanayochimbwa nchini Malawi, yakiwemo lakini si tu uraniamu, madini adimu, niobamu, grafiti, tantalum, bauxite, makaa ya mawe, chokaa, vito, mchanga mzito wa madini, vermiculite, fosfeti, pyrite rutile, dhahabu, almasi, shaba, n.k." inasema amri tendaji hiyo ya tarehe 23 Oktoba, 2025, na iliyosainiwa na Rais Mutharika.

“Mtu au chombo chochote kitakachobainika kukiuka amri tendaji hiyo kitakabiliwa na adhabu, faini, na vikwazo vingine kama ilivyoainishwa na sheria za Malawi.” Amri tendaji hiyo inasema.

Hata hivyo, marufuku hiyo, haihusu madini ambayo yameshachakatwa, kusafishwa, au kutengenezwa kuwa bidhaa zenye thamani ya nyongeza nchini Malawi kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya madini.

Rais Mutharika amesema utekelezaji wa amri hiyo utapitiwa na kufuatiliwa mara kwa mara ili kutathmini athari zake kwa uchumi, viwanda, na mazingira, huku wizara inayohusika na madini ikihitajika kuwasilisha ripoti kwa rais kuhusu mwenendo ya utekelezaji wake.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha