Lugha Nyingine
Mwakilishi wa Rais wa China ahudhuria hafla ya kuapishwa kwa rais wa Ushelisheli
Mwakilishi Maalum wa Rais Xi Jinping wa China, Gao Yunlong, amehudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Ushelisheli Patrick Herminie iliyofanyika Jumapili mjini Victoria na kufanya mazungumzo na rais huyo baada ya hafla hiyo
Katika mazungumzo hayo, Rais Herminie amepongeza mapendekezo ya dunia yaliyotolewa na Rais Xi Jinping, akisema kuwa nchi yake itaendelea kushikilia kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja, na kuimarisha ushirikiano wa kivitendo na China ndani ya mifumo kama vile Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, ili kuboresha maendeleo ya uhusiano wa pande mbili.
Kwa upande wake, Gao Yunlong amewasilisha salamu za rais huyo wa China, na kusema China inaweka umuhimu mkubwa katika maendeleo ya uhusiano kati yake na Ushelisheli, na iko tayari kufanya kazi na Ushelisheli kutimiza utekelezaji wa matokeo ya mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika mjini Beijing.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



