Rais aliyeko madarakani wa Cote d’Ivoire ashinda uchaguzi wa rais

(CRI Online) Oktoba 28, 2025

Picha iliyopigwa Oktoba 25, 2025, ikimuonyesha Rais Alassane Ouattara akiwa kwenye kituo cha kupigia kura, mjini Abidjan, Cote d'Ivoire. (Xinhua/Zhang Jian)

Picha iliyopigwa Oktoba 25, 2025, ikimuonyesha Rais Alassane Ouattara akiwa kwenye kituo cha kupigia kura, mjini Abidjan, Cote d'Ivoire. (Xinhua/Zhang Jian)

Rais aliyeko madarakani sasa wa Cote d'Ivoire, Alassane Ouattara wa chama cha Rally of Houphouetists for Democracy and Peace, ameshinda awamu ya nne katika uchaguzi wa rais kwa kupata asilimia 89.77 ya kura zote halali zilizopigwa.

Kwa mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi ya nchini humo, Ouattara amepata kura milioni 3,759,030 kati ya jumla ya kura 4,187,318 halali zilizopigwa, huku idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura ikifikia asilimia 50.10 kati ya watu milioni 6.7 waliojiandikisha kupiga kura ndani na nje ya Cote d’Ivoire.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha