Lugha Nyingine
Mji wa kale wa Zhuoshui watumia maliasili kuhimiza maendeleo ya shughuli za utalii wa kitamaduni katika Mji wa Chongqing, China (3)
![]()  | 
| Watalii wakipiga picha kwenye mji wa kale wa Zhuoshui katika Eneo la Qianjiang, Mji wa Chongqing, kusini magharibi mwa China, Oktoba 30, 2025. (Xinhua/Tang Yi) | 
Mji wa kale wa Zhoushui upo katika Eneo la Qianjiang la Mji wa Chongqing, kusini magharibi mwa China, ni mji wenye historia ya miaka elfu moja, ulianzishwa mwishoni mwa Enzi ya Tang (618-907) na kustawi wakati wa enzi za Ming na Qing (1368-1911).
Ukiwa ni eneo la vivutio vya utalii la daraja la 5A la kitaifa nchini China, mji huo wa kale wa Zhuoshui umehifadhi mpangilio wake wa ujenzi wa jadi na majengo ya kipekee ya mtindo ambao ni mafungamano ya ujenzi wa majengo wa makabila ya Watujia na Wahui.
Katika miaka ya hivi karibuni, mji huo wa kale pia umetumia vya kutosha maliasili zake na utamaduni wake kuhimiza maendeleo ya shughuli za utalii wa kitamaduni wa eneo hilo. Takwimu zinaonyesha kuwa eneo hilo la vivitio vya utalii liliwapokea watalii kwa mara zaidi ya milioni 5 kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu, likipata mapato ya utalii ya yuan milioni 110 kwa jumla (dola za Kimarekani karibu milioni 15.5)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




