Wateja wafanya manunuzi kwenye jengo la maduka mengi yasiyotozwa ushuru mjini Sanya, Mkoa wa Hainan, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 10, 2025
Wateja wafanya manunuzi kwenye jengo la maduka mengi yasiyotozwa ushuru mjini Sanya, Mkoa wa Hainan, China
Wateja wa kigeni wakinunua bidhaa kwenye kwenye jengo la maduka mengi yasiyotozwa ushuru mjini Sanya, Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, Novemba 9, 2025. (Xinhua/Guo Cheng)

Forodha ya Mji wa Haikou katika Mkoa wa Hainan, kusini mwa China imesimamia jumla ya yuan milioni 506 (dola za Kimarekani karibu milioni 71) katika mauzo yasiyotozwa ushuru kutoka kwa wanunuzi takriban 72,900 katika wiki ya kwanza (kuanzia Novemba 1 hadi 7) ya utekelezaji wa sera iliyopanuliwa ya kutotoza ushuru kwa bidhaa zinazonunuliwa na wateja kabla ya kuondoka kisiwa hicho. Takwimu hizi zimefikia ongezeko la asilimia 34.86 zikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana katika thamani ya mauzo, ambapo idadi ya wanunuzi imeongezeka kwa asilimia 3.37.

Mkoa huo wa kisiwa wa Hainan ulipanua wigo wa bidhaa zake zisizotozwa ushuru za kupelekwa nje ya nchi kwa kuongeza aina mbili mpya za bidhaa, yaani vitu vya wanyama vipenzi wa kuishi na binadamu na ala za muziki zinazobebeka. Baada ya marekebisho hayo yaliyoanza kufanya kazi Novemba 1, orodha ya kisiwa hicho ya vitu vinavyonunuliwa na wateja bila kutozwa ushuru kabla ya kuondoka kisiwa hicho imehusisha aina 47 za bidhaa.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha