Taarifa rasmi yathibitisha vifo vya watu wanane kwenye mlipuko uliotokea Delhi, India

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 11, 2025

Polisi, askari wa zimamoto na waandishi wa habari wa India wakiwa wamekusanyika kwenye eneo la mlipuko wa gari karibu na Red Fort mjini New Delhi, India, Novemba 10, 2025. (Str/Xinhua)

Polisi, askari wa zimamoto na waandishi wa habari wa India wakiwa wamekusanyika kwenye eneo la mlipuko wa gari karibu na Red Fort mjini New Delhi, India, Novemba 10, 2025. (Str/Xinhua)

NEW DELHI - Watu wanane kati ya wale waliopelekwa hospitalini baada ya mlipuko uliotokea mjini Delhi, India jana Jumatatu jioni wamefariki dunia, msimamizi wa matibabu wa hospitali amethibitisha ambapo hospitali hiyo pia imesema kwamba, jumla ya watu saba waliojeruhiwa bado wamelazwa hospitalini, na watatu kati yao wako katika hali mahututi.

Mlipuko huo umetokea ndani ya gari karibu na jengo la kihistoria la Red Fort. Kwa mujibu wa polisi, gari lililokuwa likiendeshwa polepole lilisimama kwenye taa nyekundu barabarani, na kisha mlipuko ukatokea. Mlipuko huo ulisababisha moto kwenye magari yaliyokuwa karibu, na kuharibu karibu magari ishirini.

Mara tu baada ya mlipuko huo, askari wa zimamoto, timu za polisi na wataalamu wa uchunguzi wa jinai walifika mahali hapo kuchunguza mlipuko huo.

Shirika kuu la uchunguzi wa ugaidi la India, Shirika la Kitaifa la Uchunguzi (NIA), na Shirika la Walinzi wa Usalama wa Taifa (NSG) zimejiunga kwenye uchunguzi wa tukio hilo.

"Baada ya mlipuko huo mbaya nje ya stesheni ya metro ya Red Fort mjini Delhi Jumatatu jioni, tahadhari kubwa imetolewa katika mji mkuu wa nchi hiyo. Mji mkuu wa kibiashara wa India, Mumbai, pia, umewekwa katika tahadhari kubwa kufuatia mlipuko huo mjini Delhi," imesema kituo cha televisheni cha India Today.

Imeripoti kwamba mlipuko huo mjini Delhi umesababisha mamlaka katika miji na majimbo kadhaa, yakiwemo ya Kolkata, Dehradun, Haryana, na Uttar Pradesh, kutangaza hali ya tahadhari na kuimarisha hatua za usalama.

Kituo kingine cha televisheni NDTV kimesema idadi ya watu waliofariki kuwa ni 13.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ameomboleza vifo hivyo. Waziri wa Mambo ya Ndani wa India Amit Shah alitembelea hospitali ambako majeruhi wamelazwa.

Vikosi vya mabomu na timu za uchunguzi wa jinai zilifika eneo husika ili kubaini aina ya vilipuzi vilivyotumika katika mlipuko huo. Juhudi pia zimefanywa kumtafuta mmiliki wa gari lililotumika kwenye mlipuko huo. 

Polisi na askari wa zimamoto wa India wakiwa wamekusanyika kwenye eneo la mlipuko wa gari karibu na Red Fort mjini New Delhi, India, Novemba 10, 2025. (Str/Xinhua)

Polisi na askari wa zimamoto wa India wakiwa wamekusanyika kwenye eneo la mlipuko wa gari karibu na Red Fort mjini New Delhi, India, Novemba 10, 2025. (Str/Xinhua)

Ambulensi zikiwa zimepanga foleni kwenye eneo la mlipuko wa gari karibu na Red Fort mjini New Delhi, India, Novemba 10, 2025. (Str/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha