Wataalamu watoa wito wa ushirikiano imara kati ya G20 na Afrika juu ya uendelevu wa madeni

(CRI Online) Novemba 11, 2025

Mazungumzo ya ngazi ya juu ya kati ya Kundi la 20 (G20) na Afrika juu ya uendelevu wa madeni, gharama ya mtaji, na mageuzi ya ufadhili yamefanyika jana Jumatatu mjini Addis Ababa, Ethiopia, yakitoa wito wa kuimarisha ushirikiano.

Mkutano huo, uliandaliwa na Nchi Mwenyekiti wa Zamu wa G20, Afrika Kusini, kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika (AU) kwenye makao makuu ya AU, mjini Addis Ababa.

Kamishna wa Maendeleo ya Uchumi, Biashara, Utalii, Viwanda, na Madini wa AU Francisca Tatchouop Belobe amesema kwamba uhimilivu wa mataifa ya Afrika unajaribiwa na mzigo wa madeni usio endelevu na mfumo wa kifedha unaoiadhibu Afrika.

Ametoa wito wa ushirikiano ambao unaichukulia Afrika siyo kama hatari inayohitaji kusimamiwa, bali kama mshirika wa kuwezeshwa. Pia ameelezea mipango ya AU, ikiwa ni pamoja na juhudi za kuanzisha utaratibu wa ufuatiliaji wa madeni ya Afrika kwa uwazi wa mambo ya kifedha na uhuru wa kifedha wa Afrika.

Naye Naibu Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini Alvin Botes amesisitiza uharaka wa mazungumzo kushughulikia moja ya vipaumbele vikuu yaani kuhakikisha uendelevu wa madeni kwa nchi zenye kipato cha chini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha