Lugha Nyingine
Iran yakataa shutuma za NATO za kushirikiana na Russia kuharibu sheria za kimataifa

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baghaei akihudhuria mkutano wa waandishi wa habari mjini Tehran, Iran, Novemba 10, 2025. (Xinhua/Shadati)
TEHRAN - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baghaei amekataa kauli za hivi karibuni za Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO) Mark Rutte zilizoishutumu Iran na Russia kushirikiana kuharibu sheria za kimataifa.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari wa kila wiki juzi Jumatatu, Baghaei alisema kwamba hatua nyingi zinazochukuliwa na nchi wanachama wa NATO ni zile zinazozishutumu nchi nyingine kuzichukua, na kwamba ukiangalia ukweli, inaonyesha ni upande gani umekiuka sheria za kimataifa na Katiba ya Umoja wa Mataifa, Iran au nchi wanachama wa NATO.
Akitolea mfano wa Marekani kuivamia na kuikalia kimabavu Afghanistan na "uhalifu" wake katika nchi hiyo, amesema katika mwaka uliopita, ukiukaji wa sheria na wa sheria za kimataifa uliofanywa na Marekani na baadhi ya nchi wanachama wengine wa NATO umegeuka kuwa mfano unaojirudia.
Baghaei amesema Marekani, "ikiwa ni nchi mwanachama mwenye ushawishi mkubwa zaidi wa NATO," ni mvurugaji wa amani na usalama wa kimataifa, akisisitiza kwamba kauli hizo za mkuu wa NATO zilikuwa tu "mchezo na shutuma zisizo na maana dhidi ya Iran."

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baghaei akihudhuria mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran, Iran, Novemba 10, 2025. (Xinhua/Shadati)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



