Nchi za Afrika zaahidi kuboresha uzalishaji wa bidhaa za afya

(CRI Online) Novemba 12, 2025

Nchi za Afrika jana Jumanne kwenye Mkutano wa 7 wa Kisayansi juu ya Udhibiti wa Bidhaa za Matibabu Barani Afrika (SCoMRA VII) unaofanyika mjini Mombasa, Kenya zimekubaliana kuimarisha uratibu katika utafiti wa bidhaa za afya, uzalishaji, na udhibiti ili kuboresha uzalishaji wa ndani na kupunguza utegemezi kutoka nje.

Kwenye mkutano huo ambao hufanyika kila baada ya miaka miwili, wajumbe wamejadiliana kuhusu dharura inayozidi kuongezeka ya kukabiliana na udhaifu uliodhihirishwa na dharura kama mlipuko wa Ebola na COVID-19.

Mwenyekiti wa Bodi ya Madawa na Sumu ya Kenya John Munyu amesema, kufungua uwezo bora wa Afrika katika utengenezaji na biashara ya bidhaa za afya ni kipaumbele kikubwa cha bara hilo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha