Lugha Nyingine
Spishi mpya ya chura yagunduliwa katika Mkoa wa Guangdong, China, na kupewa jina la “kung fu”

Picha iliyopigwa Aprili 29, 2025 ikionesha “Leptobrachella Kungfu”, spishi mpya ya chura iliyogunduliwa mjini Foshan, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China. (Xinhua)
Spishi mpya ya chura imegunduliwa mjini Foshan, Guangdong, Kusini mwa China. Imepewa jina la “Leptobrachella Kungfu”, lililohamasishwa kutokana na sanaa ya Kung Fu ya China, na kuenzi urithi wa utamaduni wa mji huo wa Foshan unaojulikana sana kwa jina la “Mji wa Kung Fu.”
Ugunduzi huo, uliofanywa kwa pamoja na watafiti kutoka Chuo cha Ufundi cha Uhandisi wa Ulinzi wa Mazingira ya Asili na Akademia ya Guangdong ya Sayansi ya Mazingira ya Asili, umechapishwa jana Jumatano kwenye jarida la kimataifa la taxonomic “ZooKeys.”
Timu hiyo ya utafiti imesema, imegundua kwamba, spishi hiyo mpya ni ndogo kwa umbo, huku sampuli za vyura sita madume wazima waliokusanywa wakiwa na kipimo cha kutoka milimita 25.7 hadi 28.2 katika urefu wa sehemu ya pua.
Chura hao wana mstari dhahiri mweusi nyuma ya macho, vidole vyenye utando wa ngozi wa kiasi kidogo kati yake na ukingo mnene.
Spishi hiyo inapatikana hasa katika maeneo ya vilima vya Magharibi mwa Eneo la Ghuba Kubwa ya Guangdong-Hong Kong-Macao, ambalo lina idadi kubwa ya wakazi na maendeleo ya mji ya kiwango cha juu.

Picha iliyopigwa Apirli 29, 2025 ikionesha “Leptobrachella Kungfu”, spishi mpya ya chura iliyogunduliwa mjini Foshan, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China. (Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



