Lugha Nyingine
Cambodia yasema askari wa Thailand wamewafyatulia risasi raia wa Cambodia na kusababisha watu watano kujeruhiwa

Mwanaume aliyejeruhiwa, wa pili kutoka kulia, akiwa amechukuliwa na askari wa Jeshi la Cambodia aliyepanda pikipiki baada ya askari wa Thailand kuwafyatulia risasi raia katika Kijiji cha Prey Chan, Jimbo la Banteay Meanchey, kwenye mpaka na Thailand, Jumatano, Novemba 12, 2025. (Picha/cfp)

Madaktari wa Cambodia wakimhudumia mwanaume aliyejeruhiwa kutokana na mgogoro uliotokea kwa mara nyignine tena kati ya Cambodia na Thailand kwenye eneo la mpakani katika Jimbo la Banteay Meanchey la Cambodia, Novemba 12, 2025. (Picha/cfp)
PHNOM PENH - Waziri wa Upashanaji Habari wa Cambodia Neth Pheaktra amesema, askari wa Thailand wamefyatulia risasi dhidi ya wanakijiji wa Cambodia katika mgogoro unaoendelea wa kugombania mpaka, na kusababisha watu watano kujeruhiwa.
Kwa kupitia habari zilizotolewa na Telegram kwa waandishi wa habari, Waziri huyo amesema jana Jumatano, "Serikali ya Cambodia imepata habari kwa hatua ya kwanza zikisema kuwa, Askari wa Thailand wamefyatulia risasi dhidi ya raia katika kijiji cha Prey Chan cha Komuna ya Ou Beychoan ya eneo la Ou Chrov katika jimbo la Banteay Meanchey, na kusababisha raia watano kujeruhiwa”.
Tukio hilo limetokea siku mbili baada ya Waziri Mkuu wa Thailand Anutin Charnvirakul kuamuru kusitishwa kwa Taarifa ya pamoja ya Amani, kufuatia mlipuko wa bomu la ardhini karibu na hekalu la Preah Vihear kwenye eneo la mpakani, ambao umesababisha askari wawili wa Thailand kujeruhiwa.
Thailand imeishutumu Cambodia kwa kutega mabomu mapya ardhini, lakini Cambodia imekana madai hayo ya Thailand, ikisema kwamba mabomu hayo yaliachwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Cambodia karibu miaka 30 iliyopita.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



