Peng Liyuan na Malkia Letizia wa Hispania watembelea kituo cha kuwahudumia watu wenye ulemavu mjini Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 13, 2025

Peng Liyuan, Mke wa Rais wa China Xi Jinping, na Malkia Letizia wa Hispania wakifahamishwa kuhusu shughuli za kusomea kwa watoto wenye ulemavu katika eneo la kusomea lisilo la faida la Kituo cha Kielelezo cha kuwahudumia Watu Wenye Ulemavu cha Beijing mjini Beijing, mji mkuu wa China, Novemba 12, 2025. (Xinhua/Ding Lin)

BEIJING - Peng Liyuan, Mke wa Rais wa China Xi Jinping, na Malkia Letizia wa Hispania, ambaye ameambatana na Mfalme Felipe wa VI wa Hispania katika ziara yake rasmi nchini China, wametembelea Kituo cha Kielelezo cha kuwahudumia Watu Wenye Ulemavu cha Beijing jana Jumatano.

Wakiwa kwenye kituo hicho, Peng na Letizia walisikiliza ufahamisho wa miradi ya huduma kwa watu wenye ulemavu na kutembelea maonyesho yenye mada maalumu kuhusu Michezo ya Majira ya Baridi ya Paralimpiki ya Beijing 2022.

Kisha walielekea kwenye ukumbi wa maonyesho wa bidhaa za teknolojia ya juu za kuwasaidia watu wenye ulemavu na eneo la kusomea lisilo la faida, ambapo walifahamishwa kuhusu matumizi ya bidhaa za kusaidia watu wenye ulemavu, shughuli za kusomea kwa watoto wenye ulemavu, na uwekaji wa vifaa visivyo na vizuizi nchini China.

Peng na Letizia walikuwa na mazungumzo ya kirafiki na watu wenye ulemavu waliokuwa wakishiriki kwenye mafunzo ya ujuzi wa kuoka mikate, utengenezaji wa kazi za mikono na uchoraji kwenye kituo hicho.

Pia walitembelea watoto wenye ulemavu waliokuwa wakipata mafunzo ya kurejesha kawaida afya ya mwili. Katika mazingira ya upendo na ya kirafiki, watoto hao wenye ulemavu wa kuona kwenye kituo hicho waliimba wimbo wa Kichina, Nyimbo na Tabasamu, kwa ajili ya wageni hao waliowatembelea.

Peng amesema kwamba maendeleo ya watu wenye ulemavu yanahitaji juhudi na uungaji mkono wa pamoja kutoka kwa pande zote ili kuwasaidia kujiunga vyema zaidi katika jamii.

Ameelezea matumaini kwamba China na Hispania zitaimarisha mawasiliano na ushirikiano ili kusaidia kutimiza ndoto za watu wenye ulemavu.

Kwa upande wake Malkia Letizia ameuliza kwa undani kuhusu maendeleo ya kazi za China kwa watu wenye ulemavu, hasa hali ya ajira kwa wanawake wenye ulemavu, na amepongeza sana mafanikio ambayo China imepata katika eneo hilo.

Peng Liyuan, Mke wa Rais wa China Xi Jinping, na Malkia Letizia wa Hispania wakipiga picha ya pamoja na watu wenye ulemavu wanaojishughulisha na utengenezaji wa kazi za mikono kwenye Kituo cha Kielelezo cha kuwahudumia Watu Wenye Ulemavu cha Beijing mjini Beijing, mji mkuu wa China, Novemba 12, 2025. (Xinhua/Li Xiang)

Peng Liyuan, Mke wa Rais wa China Xi Jinping, na Malkia Letizia wa Hispania, ambaye ameambatana na Mfalme Felipe wa VI wa Hispania katika ziara yake nchini China, wakitembelea Kituo cha Kielelezo cha kuwahudumia Watu Wenye Ulemavu cha Beijing mjini Beijing, mji mkuu wa China, Novemba 12, 2025. (Xinhua/Li Xiang)

Peng Liyuan, Mke wa Rais wa China Xi Jinping, na Malkia Letizia wa Hispania, wakitazama watoto wenye ulemavu wa kuona wakiimba wimbo wa Kichina, Nyimbo na Tabasamu, kwenye Kituo cha Kielelezo cha kuwahudumia Watu Wenye Ulemavu cha Beijing mjini Beijing, mji mkuu wa China, Novemba 12, 2025. (Xinhua/Zhai Jianlan)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha