Lugha Nyingine
Uchumi wa uvuvi wa baharini wastawi katika Mkoa wa Shandong wa China (2)
Mkoa Shandong, mashariki mwa China ukiwa ni mkoa unaojulikana sana kwa uchumi wake wa uvuvi wa baharini, umekuwa ukifanya juhudi kubwa za kujenga vituo vya ufugaji samaki baharini katika miaka ya hivi karibuni, ukilenga kutajirisha hatua kwa hatua "ghala la chakula cha baharini."
Hadi sasa, mkoa huo wa Shandong umeshajenga " vituo 139 vya ufugaji samaki baharini" vya ngazi ya mkoa au vya ngazi ya juu, kati yake vituo 71 ni vya ngazi ya kitaifa, ambavyo vinachukua asilimia 38 ya vituo vya ngazi hiyo vya jumla vya kote nchini . Mkoa huo sasa umekuwa na mnyororo kamili wa shughuli za kutoka ufugaji wa samaki, uvuvi hadi utengenezaji wa kina wa mazao ya samaki. Uzalishaji wa mazao ya baharini katika mkoa huo wa Shandong ulifikia tani milioni 8.25, thamani ya uzalishaji iliyoongezwa ikizidi yuan bilioni 100 (dola za Kimarekani karibu bilioni 14.09) mwaka 2024, ukiongoza uzalishaji huo katika mikoa yote nchini China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




