Lugha Nyingine
Mkutano wa Ushirikiano kati ya China na Afrika waangazia ushirikiano kuelekea usimamizi wa pamoja wa dunia (4)
![]() |
| Wajumbe wakihudhuria Mkutano wa Ushirikiano kati ya China na Afrika wa Jukwaa la Vyombo vya Habari na Majopo ya Washauri Bingwa la Nchi za Kusini mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Novemba 13, 2025. (Xinhua/Chen Wei) |
JOHANNESBURG - Mkutano wa Ushirikiano kati ya China na Afrika wa Jukwaa la Vyombo vya Habari na Majopo ya Washauri Bingwa la Nchi za Kusini umefunguliwa rasmi jana Alhamisi mjini Johannesburg, Afrika Kusini ili kuchunguza njia za kuimarisha ushirikiano, kupaza sauti ya pamoja ya Nchi za Kusini na kuhimiza usimamizi wa pamoja wa dunia.
Ukiwa umeandaliwa kwa pamoja na Shirika la Habari la China, Xinhua, Umoja wa Afrika (AU) na Kampuni ya Independant Media ya Afrika Kusini, pamoja na wadau wengine, mkutano huo wa siku mbili umekusanya wawakilishi zaidi ya 200 kutoka vyombo vya habari, majopo ya washauri bingwa, mashirika ya kiserikali na taasisi nyingine nyingi 160 kutoka China na nchi 41 za Afrika, pamoja na AU.
Chini ya kaulimbiu ya "Kuufanyia Mageuzi Usimamizi Duniani: Majukumu na Maono Mapya kwa Ushirikiano kati ya China na Afrika," mkutano huo unatilia maanani katika jinsi ushirikiano kati ya vyombo vya habari na majopo ya washauri bingwa unavyoweza kusaidia kujenga usimamizi duniani wenye haki na ulio jumuishi zaidi.
Kwenye hotuba yake kuu katika hafla ya ufunguzi, Lyu Yansong, mhariri mkuu wa Xinhua, amesema kwamba Rais Xi Jinping wa China ametoa kipaumbele kwenye ushirikiano kati ya China na Afrika, na katika Mkutano wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) mwezi Septemba mwaka jana, Rais Xi alipendekeza kuinua kiwango cha uhusiano kati ya China na Afrika hadi kwenye jumuiya ya hali zote ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja kwa zama mpya.
"Tunapaswa kutoa mchango wa hekima yetu katika kulifanya Kundi la Nchi za Kusini kuwa nguvu ya kuleta utulivu kwa ajili ya kulinda amani, nguzo ya maendeleo ya wazi, nguvu ya kiujenzi katika usimamizi duniani, na nguvu ya kuhimiza kwa ajili ya kufunzana miongoni mwa ustaarabu." Lyu amesema akiongeza kuwa vyombo vya habari na majopo ya washauri bingwa zinabeba jukumu muhimu la kusambaza taarifa za kuaminika na kurekodi matukio ya nyakati.
Mhariri mkuu huyo wa Xinhua amependekeza kutekeleza Pendekezo la Maendeleo Duniani, Pendekezo la Usalama Duniani, Pendekezo la Ustaarabu Duniani na Pendekezo la Usimamizi Duniani.
Iqbal Surve, mwenyekiti wa Independent Media ya Afrika Kusini, amepongeza ushirikiano kati ya Afrika na China akiuelezea kuwa ni mwanga unaoonyesha kile ushirikiano wa kweli unaweza kufikia, uliojengwa juu ya msingi wa kuheshimiana, malengo ya pamoja, na dhamira ya kujenga utaratibu wa dunia ulio wa haki na jumuishi zaidi.
Katika hotuba yake, Leslie Richer, mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa AU, amesema kwamba utaratibu wa kimataifa unabadilika huku kukiwa na wito unaoongezeka kutoka Nchi za Kusini wa uwakilishi wa haki, udhibiti wa rasilimali na maendeleo yenye heshima.
Jukwaa hilo pia linawasilisha ripoti ya majopo ya washauri bingwa yenye kichwa "Kujenga Kwa Pamoja Mfano Mpya wa Uongozi Duniani -- Kushirikiana Kutafuta Mfumo wa Usimamizi Duniani ulio wa Haki na Mantiki Zaidi," na uzinduzi wa mtandao wa ushirikiano wa mawasiliano ya Nchi za Kusini "Kuungana katika Moyo, Njia na Vitendo -- Mpango Kazi wa Uwezeshaji wa Ushirikiano kati ya China na Afrika 2026."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




