Treni za mizigo za China na Ulaya zachochea mageuzi ya Mji wa Xi'an kuwa kituo cha kisasa cha kimataifa cha biashara na usafirishaji (8)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 17, 2025
Treni za mizigo za China na Ulaya zachochea mageuzi ya Mji wa Xi'an kuwa kituo cha kisasa cha kimataifa cha biashara na usafirishaji
Picha iliyopigwa Novemba 14, 2025 ikionyesha kreni zikifanya kazi kwenye Stesheni ya Bandari ya Kimataifa ya Xi'an mjini Xi'an, Mkoani Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China. (Xinhua/Shao Rui)

Ikiwa ilizinduliwa rasmi mwaka 2013, treni za mizigo zinazotoa huduma kati ya China na Ulaya katika Mji wa Xi'an, kaskazini magharibi mwa China zimekuwa zikishikilia nafasi ya kwanza nchini kote China kwa miaka mingi katika viashiria muhimu kama vile idadi ya treni, kiasi cha mizigo na kiwango cha makontena yaliyojaa.

Kwa sasa, Stesheni ya Bandari ya Kimataifa ya Xi'an inaendesha njia 59 za reli, huku ikiwa na uwezo wa kupitisha makontena milioni 5.4 (TEUs) kwa mwaka. Miradi kama vile bandari ya Kazakhstan-Xi'an imekamilika na kuanza kufanya kazi, ikiwezesha biashara na usafirishaji kati ya Ulaya na Asia, na kuharakisha mageuzi ya mji huo kuwa kituo cha kisasa cha kimataifa cha biashara na usafirishaji.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha