Manowari ya kwanza ya kivita ya amfibia ya Aina ya 076 ya China "Sichuan" yakamilisha majaribio yake ya kwanza baharini (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 17, 2025
Manowari ya kwanza ya kivita ya amfibia ya Aina ya 076 ya China
Manowari ya kwanza ya kivita ya amfibia ya Aina ya 076 ya China, Sichuan, ikirudi kwenye gati la meli baada ya kukamilisha majaribio yake ya kwanza baharini, Novemba 16, 2025. (Picha na Zhang Liang/Xinhua)

SHANGHAI - Manowari ya kwanza ya kivita ya amfibia Aina ya 076 ya China, Sichuan, imerudi kwenye gati la meli mjini Shanghai, mashariki mwa China majira ya saa 11 jioni jana Jumapili baada ya kukamilisha majaribio yake ya kwanza baharini.

Zoezi hilo la siku tatu lilipima mifumo ya usukumo na umeme ya manowari iliyoundwa na China yenyewe, pamoja na vifaa vingine, ikipata matokeo yaliyotarajiwa.

Manowari hiyo ya Sichuan itaendelea majaribio mengine yatakayofuata kulingana na mipango iliyowekwa.

Ikiwa ni manowari ya kizazi kipya ya kivita ya amfibia ya Kikosi cha Majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), manowari hiyo inajumuisha teknolojia za kiuvumbuzi za sumakuumeme ya kuwezesha ndege kutua na kupaa, ikiiwezesha kubeba ndege za mabawa yasiyoweza huhamishika, helikopta na vifaa vya amfibia.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha