Lugha Nyingine
Rais Xi akutana na mfalme wa Tonga, akihimiza kuhusishana vizuri mikakati ya maendeleo (3)
![]() |
| Rais wa China Xi Jinping akifanya hafla ya kumkaribisha Mfalme Tupou VI wa Ufalme wa Tonga, kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing Novemba 25, 2025. (Xinhua/Ding Haitao) |
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Mfalme Tupou VI wa Ufalme wa Tonga aliyeko ziarani mjini Beijing, China jana Jumanne, akisema kwamba China ina nia ya kuongeza kuhusishana kwa mikakati ya maendeleo na Tonga.
Rais Xi akidhihirisha kuwa China na Tonga ni marafiki wa kweli ambao wamepitia dhoruba na kuvumilia magumu pamoja, tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, nchi hizo mbili zimekuwa zikiungana mkono kithabiti katika maslahi ya kimsingi na mambo yanayofuatiliwa na kila mmoja.
"Ushirikiano wa kivitendo umepata matunda kemkem, na uhusiano wa kiwenzi wa kimkakati kwa pande zote kati ya China na Tonga umeimarishwa kwa kina siku hadi siku, na hivyo kuweka mfano wa urafiki na ushirikiano kati ya nchi zenye mifumo tofauti ya jamii, na kati ya nchi zenye tofauti kwa ukubwa," amesema Rais Xi, akiongeza kuwa bila kujali namna hali ya kimataifa inavyobadilika, China imekuwa mshirika wa kuaminika na mzuri wa Tonga na siku zote imekuwa ikiiunga mkono Tonga katika kulinda uhuru na mamlaka yake ya nchi.
Rais Xi amesema China ina nia ya kupanua ushirikiano na Tonga katika biashara na uwekezaji, kilimo na uvuvi, miundombinu, nishati safi, huduma za matibabu na afya, utalii, na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
"China pia itazidisha mawasiliano katika sekta za elimu, michezo, vijana, vyombo vya habari, na ushirikiano kati ya serikali za mitaa, na kuendelea kutoa msaada kwa maendeleo ya uchumi na jamii ya Tonga ndani ya mfumo wa ushirikiano wa Kusini na Kusini." Amesisitiza kuwakaribisha watu kutoka sekta mbalimbali za Tonga kutembelea China na kubadilishana mawazo kuhusu utawala wa nchi na uzoefu wa kujiendeleza ili kufahamishwa na kujua zaidi kuhusu China.
"China pia inapenda kushirikiana na Tonga katika kutekeleza mapendekezo makuu manne kwa dunia , kutoa maisha bora kwa watu wa nchi zote mbili, kujenga jumuiya ya China na nchi za Visiwa vya Pasifiki yenye mustakabali wa pamoja, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja," Rais Xi amesema.
Mfalme Tupou VI akitoa shukrani kwa msaada wa muda mrefu na usio na ubinafsi wa China katika maendeleo ya uchumi na jamii ya Tonga, amesema Tonga inaweka umuhimu mkubwa katika kuendeleza uhusiano na China.
Mfalme huyo ameongeza, "Tonga inafuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja, inapinga 'kujitenga kwa Taiwan' kwa namna yoyote ile, na inaunga mkono waziwazi juhudi za serikali ya China kwa ajili ya muungano wa taifa.”
Kabla ya mkutano huo, Rais Xi na mkewe, Peng Liyuan, walifanya hafla ya makaribisho kwa ajili ya Mfalme Tupou VI na Malkia Nanasipau'u kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.
Rais Xi na Peng waliandaa karamu ya kuwakaribisha Mfalme na Malkia wakati wa alasiri.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




