Lugha Nyingine
Handaki la Jingu Haihe kwenye njia ya Reli ya Mwendokasi ya Tianjin-Weifang lakamilika kuchimbwa kwa mafanikio
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 28, 2025
Handaki la Jingu Haihe kwenye njia ya Reli ya Mwendokasi ya Tianjin-Weifang mjini Tianjin, kaskazini mwa China limekamilika kuchimbwa kwa mafanikio jana Alhamisi.
Handaki hilo la Jingu Haihe lenye urefu wa kilomita 6.7 ni handaki pekee kwenye njia nzima ya reli hiyo, likiwa na kipenyo cha juu cha kuchimbwa kinachofikia mita 13.8. Pia ni handaki la kwanza la reli ya mwendokasi kuvuka Mto Haihe.
Reli ya Tianjin-Weifang itakapokamilika itaunganisha Stesheni ya Reli ya Binhai mjini Tianjin na Stesheni ya Reli ya Weifang Kaskazini katika Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China. Njia hiyo ya reli ina urefu wa kilomita takriban 349 na uendeshaji wa treni umesanifiwa kwa kasi ya kilomita 350 kwa saa.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




