Lugha Nyingine
Treni ya kwanza ya Laos yafanya usafirishaji wa wanga wa muhogo kuelekea kuuzwa China (3)
VIENTIANE - Treni ya kusafirisha makontena yanayobeba tani 1,000 za wanga wa muhogo tu imeondoka kutoka Stesheni ya Reli ya Vientiane Kusini kwenye Reli ya China-Laos juzi Jumamosi, na inatazamiwa kuwasili Zhengzhou, mkoani Henan, China ndani ya muda wa saa 80. Hii ni mara ya kwanza kwa wanga wa muhogo kutoka Laos kusafirishwa kuuzwa China.
Tani hizo 1,000 za wanga wa muhogo zimezalishwa na kiwanda cha utengenezaji wa wanga wa muhogo cha Laos.
Mzigo huo umeandaliwa na Kampuni ya Shirika la Reli la China ya Kusafirisha Makontena, Kampuni ya Treni ya China-Ulaya imekabidhiwa kazi ya usafirishaji wa bihaa, ambapo ikitoa huduma kwa wateja katika mchakato kamili wa kupanga usafirishaji, muundo wa kupakia makontena, uchukuaji na uwasilishaji wa bidhaa, utayarishaji wa bili za njiani, ufuatiliaji wa taarifa na huduma za kukabiliana na dharura.
Kampuni ya Reli ya Laos-China (LCRC), ambayo inaendesha sehemu ya Laos ya Reli ya China-Laos, imesema kwamba tangu reli hiyo izinduliwe, imewapa wauzaji nje wa mazao ya kilimo wa Laos rasilimali za makontena zenye ubora wa juu na uwezo wa usafirishaji wa kuaminika, na kuhakikisha bidhaa zinawasilisha kwa wakati.
Kampuni hiyo imesema, hadi sasa, imeshughulikia tani zaidi ya milioni 16 za mizigo, ikiwa ni pamoja na tani zaidi ya milioni 1.7 za bidhaa za kilimo zilizosafirishwa kuuzwa China.
Katika siku za baadaye, kampuni hiyo itaendelea kufanya kazi kwa karibu na idara za reli za China ili kuendesha treni za mizigo zinazobeba wanga wa muhogo na mazao mengine ya kilimo kwa ratiba maalum, kuandaa njia salama, yenye ufanisi, na ya ubora wa juu kwa ajili ya kusafirisha nje mazao ya kilimo ya Laos.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




