Lugha Nyingine
Kenya yazindua programu ya mafunzo kwa walimu wenyeji wa lugha ya Kichina (2)
Programu ya mafunzo kwa walimu wenyeji wa lugha ya Kichina imezinduliwa jana Jumapili jijini Nairobi, mji mkuu wa Kenya ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhimiza uhusiano wa kiutamaduni kati ya China na Kenya.
Maafisa wa serikali, wahadhiri na wanafunzi kutoka China na Kenya walihudhuria zoezi la mafunzo ya siku tatu kwa wanafunzi 170, ambayo yaliandaliwa na Kituo cha Elimu na Ushirikiano wa Lugha (CLEC) cha Wizara ya Elimu ya China, Chuo Kikuu cha Ualimu cha Tianjin, na Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Nairobi.
Katibu wa elimu ya juu na utafiti katika Wizara ya Elimu ya Kenya, Carol Wangui Hunja, amesema programu hiyo ya mafunzo imeandaliwa ili kuunga mkono juhudi za nchi hiyo za kupanua elimu ya lugha ya Kichina katika mtaala wa shule.
"Uwepo unaoongezeka wa lugha ya Kichina nchini Kenya utawezesha raia kutafuta ajira katika sehemu mbalimbali za dunia ambako lugha hiyo inazungumzwa" ameongeza.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa CLEC, Yu Yunfeng, amesema maendeleo ya elimu ya lugha ya Kichina nchini Kenya yamewezekana kutokana na umakini wa hali ya juu wa serikali zote mbili pamoja na uungwaji mkono mkubwa kutoka sekta zote nchini China na Kenya.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




