Lugha Nyingine
Uchumi wa wanyama kipenzi waendelea kwa kasi katika wilaya ya Caoxian mkoani Shandong, China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 01, 2025
![]() |
| Mkazi akitazama mavazi ya wanyama kipenzi wa binadamu katika Wilaya ya Caoxian, mashariki mwa Mkoa wa Shandong, China, Novemba 29, 2025.(Xinhua/Guo Xulei) |
Katika miaka ya hivi karibuni, Wilaya ya Caoxian, mashariki mwa Mkoa wa Shandong, China imetekeleza kwa kasi mpango wake wa uchumi wa wanyama kipenzi wa binadamu katika juhudi kubwa ya kuelekea kuwa kituo kikubwa zaidi duniani cha bidhaa za wanyama kipenzi wa binadamu.
Kwa sasa, wilaya hiyo ya Caoxian imeanzisha mnyororo kamili wa viwanda unaohusu samani za nyumbani za wanyama kipenzi, chakula, mavazi na zaidi. Katika miezi kumi ya kwanza mwaka huu, jumla ya thamani ya uchumi wa wanyama kipenzi wa binadamu wa wilaya hiyo ilifikia yuan bilioni 2.58 (dola za Marekani takribani milioni 365), ikiwakilisha ongezeko la asilimia 15.4 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




