Lugha Nyingine
Mkutano wa Kuifahamu China 2025 wafuatilia ujenzi wa mambo ya kisasa wa China na usimamizi duniani

Li Shulei, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC, akitoa hotuba kuu kwenye hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kuifahamu China 2025 mjini Guangzhou, Mkoani Guangdong, kusini mwa China, Desemba 1, 2025. (Xinhua/Zhang Ling)
GUANGZHOU - Mkutano wa Kuifahamu China 2025, wenye kaulimbiu ya "Mpango Mpya, Maendeleo Mapya, Machaguo Mapya – Ujenzi wa Mambo ya Kisasa wa China na Maono Mapya ya Usimamizi Duniani," umefanyika Guangzhou, mji mkuu wa Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China.
Li Shulei, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC, alihudhuria na kuhutubia hafla ya ufunguzi wa mkutano huo jana Jumatatu.
Huang Kunming, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na Katibu wa Kamati ya CPC ya Mkoa Guangdong, pia alihudhuria na kuhutubia hafla hiyo ya ufunguzi.
Wahudhuriaji wa mkutano huo wamesema kwamba baada ya miaka kadhaa ya maendeleo, Mkutano huo wa Kuifahamu China umekuwa moja ya majukwaa yenye ushawishi mkubwa kwa dunia kuifahamu China.
Wamesema kuwa, juu ya msingi wa uchunguzi na utekelezaji wa muda mrefu, China imesukuma mbele na kupanua kwa mafanikio ujenzi wa mambo ya kisasa kupitia uvumbuzi wa kinadharia na mafanikio mapya ya kivitendo tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC.
Wahudhuriaji wamesema kwamba mkutano wa nne wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC uliweka dira ya maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa wa China katika kipindi cha miaka mitano ijayo, ambayo ni yenye umuhimu mkubwa katika kutoa fursa za maendeleo na kushirikiana bega kwa bega na nchi nyingine kote duniani kwenye njia ya ujenzi wa mambo ya kisasa.
Pia wamesema kwamba ujenzi wa mambo ya kisasa wa China unafaidisha China na pia dunia.
Mkutano wa mwaka huu, ambao utafungwa leo Jumanne, umewaleta pamoja watu zaidi ya 800, wakiwemo wanasiasa, maafisa, wajasiriamali na wasomi.

Picha ikionesha tukio likifanyika kwenye Mkutano wa Kuifahamu China 2025 mjini Guangzhou, Mkoani Guangdong, kusini mwa China, Desemba 1, 2025. (Xinhua/Xiao Ennan)

Picha ikionesha hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kuifahamu China 2025 mjini Guangzhou, Mkoani Guangdong, kusini mwa China, Desemba 1, 2025. (Xinhua/Xiao Ennan)

Wahudhuriaji wakisoma vitabu kwenye Mkutano wa Kuifahamu China 2025 mjini Guangzhou, Mkoani Guangdong, kusini mwa China, Desemba 1, 2025. (Xinhua/Xiao Ennan)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



