China yaitaka Japan irejeshe kauli zenye makosa, na kukoma kukwepa wajibu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 02, 2025

BEIJING - China imeitaka Japan ijifunze masomo ya historia, ijitafakari kwa kina, ichukulie kwa uzito matakwa ya China, iondoa mara moja kauli zenye makosa bila ujanja na kuchukua hatua za kivitendo kutekeleza ahadi zake za kisiasa kwa China, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jian amesema jana Jumatatu.

"Katika masuala ya kanuni, tabia ya kukwepa wajibu haitaifikisha Japan popote," Lin amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari.

"Japan inaendelea kujificha na kukwepesha msimamo wake kuhusu suala la Taiwan. Kila inapoulizwa, Japan hata haitaji kabisa Azimio la Cairo, Tangazo la Potsdam na Nyaraka za Kujisalimisha kwa Japan -- zote ambazo zinaweka wazi kwamba Taiwan irudishwe China, wala haitaji nyaraka nne za kisiasa zinazotumika kama msingi wa kisiasa wa uhusiano kati ya China na Japan, wala ahadi ya kisiasa iliyotolewa na serikali ya Japan kuhusu kanuni ya kuwepo kwa China moja," amesema.

Lin amesema yote ambayo Japan imefanya ni kukwepa suala hilo kwa kudai kwamba msimamo wake "haujabadilika," lakini haijawahi kufafanua kikamilifu msimamo huo ni nini hasa.

"Kile ambacho Japan haitaki kufafanua si tu msimamo wake kuhusu suala la Taiwan. Desemba 1 ni maadhimisho ya miaka 82 tangu kutolewa Azimio la Cairo. Nyaraka hii, pamoja na nyaraka nyingine za sheria za kimataifa, inaeleza mamlaka ya China juu ya Taiwan, na ni matokeo muhimu ya Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti na sehemu muhimu ya utaratibu wa kimataifa wa baada ya vita." ameelezea.

Amesema Japan ina wajibu chini ya sheria ya kimataifa kuzingatia nyaraka hizo, ambazo ni sharti muhimu linaloruhusu Japan kurejeshwa kwenye jumuiya ya kimataifa baada ya Vita vya Pili vya Dunia (WWII).

"Lakini Japan haitaji hata neno moja kuhusu nyaraka hizo zenye nguvu kamili chini ya sheria ya kimataifa, na badala yake inaendelea kunukuu nyaraka inayoitenga China na baadhi ya nchi nyingine za Asia ambazo ziliteseka zaidi kutokana na uvamizi na ukoloni wa Japan," amesema.

"Hiyo ni dalili ya kusahau maumivu ya kumbukumbu ya uvamizi wa kijeshi wa Japan, kupuuza sana historia ya Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti, na changamoto ya wazi kwa mamlaka ya Umoja wa Mataifa na utaratibu wa kimataifa wa baada ya vita," amesema.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha