Iran yasema Marekani ni "tishio kubwa" kwa amani na usalama wa kimataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 02, 2025

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baghaei akihudhuria mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran, Iran, Desemba 1, 2025. (Xinhua/Shadati)

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baghaei akihudhuria mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran, Iran, Desemba 1, 2025. (Xinhua/Shadati)

TEHRAN - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baghaei amesema kwamba Marekani imekuwa "tishio kubwa" kwa amani na usalama wa kimataifa kutokana na vitendo vyake vya karibuni vya kuzilenga nchi nyingine.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Jumatatu katika mji mkuu wa Iran, Tehran, Baghaei amekosoa vitendo vya uhasama vya utawala wa Trump dhidi ya nchi kama vile Venezuela na uungaji mkono wake kwa operesheni za Israeli katika Asia Magharibi.

"Katika sehemu mbalimbali duniani, tunashuhudia vitendo vinavyotokana na msingi wa matishio na vitendo waziwazi vya nguvu kutoka Marekani. Maofisa wa Marekani walikuwa wakitoa matishio mara kwa mara dhidi ya nchi za Venezuela, Cuba, Nicaragua, na hata Brazil na Mexico zilizoko katika nusu ya Sayari ya Dunia ya Magharibi" amesema.

Baghaei pia amekosoa kitendo cha Marekani cha kutangaza anga ya Venezuela inapaswa kuchukuliwa kuwa imefungwa, akiseama hiki ni "kitendo kisichotokea hapo kabla katika historia" ambacho kinakiuka vigezo na kanuni za kimataifa, ikiwa ni pamoja na kanuni zinazohusu usalama wa usafiri wa ndege na ulinzi wa usalama. Zaidi ametaja matishio ya Trump dhidi ya nchi za Afrika, kwa mfano, Trump alitangaza kuizuia Afrika Kusini kuhudhuria kwenye mkutano wa viongozi wa G20 mwaka ujao, na huo ni mfano mwingine wa msimamo wa uhasama wa Washington.

Baghaei ameongeza kuwa uungaji mkono "kwa nguvu zote" wa Marekani juu ya vitendo vya Israeli katika Asia Magharibi, kihalisi umeifanya iwe mshirika wa "mauaji ya kimbari na ukiukaji wa mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi wa nchi za kikanda."

Pia ameikosoa Marekani kwa kuweka vizuizi vipya vya uhamiaji kwa raia kutoka nchi fulani, akisema vinaonyesha tabia ya "ubaguzi wa rangi" ya serikali ya Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza Alhamisi wiki iliyopita nia yake ya kusimamisha kabisa uhamiaji kutoka kwa nchi zile alizoziita "nchi za Dunia ya Tatu" na kutishia kufuta maamuzi ya uhamiaji yaliyotolewa na mtangulizi wake Joe Biden.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, akihudhuria mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran, Iran, Desemba 1, 2025. (Xinhua/Shadati)

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, akihudhuria mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran, Iran, Desemba 1, 2025. (Xinhua/Shadati)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha