Mkuu wa Jeshi la Sudan ataka RSF ivunjwe kama sharti la amani

(CRI Online) Desemba 02, 2025

Mkuu wa Jeshi la Sudan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Utawala wa Mpito la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan amesema kwamba mpango wowote wa amani ambao haujumuishi kuvunjwa kwa wanamgambo wa Vikosi vya Uungaji Mkono wa Haraka (RSF) "unakataliwa kabisa".

"Suluhisho pekee ni kuondolewa kwa wanamgambo" Al-Burhan amesema jana Jumatatu kwenye mkutano huko Port Sudan.

Ameahidi kulipiza kisasi dhidi ya wale aliowaelezea kuwa ni "wahalifu na wauaji", na kurejelea "umwagaji damu na mateso makubwa" katika maeneo kama Darfur na El Fasher kuwa vinapunguza suluhisho zinazowezekana.

Juhudi za upatanishi za kikanda na kimataifa, ikiwemo ile ya makubaliano ya amani ya kibinadamu ya kusimamisha mapigano kwa miezi mitatu yaliyopendekezwa hivi karibuni na Marekani, Saudi Arabia, Falme za Kiarabu, na Misri yakifuatiwa na mchakato wa kisiasa wa miezi tisa, hadi sasa zimeshindwa kupata usimamishaji mapigano.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha