Lugha Nyingine
DRC yatangaza mwisho wa mlipuko wa hivi karibuni wa homa ya Ebola

(Picha/VCG)
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imetangaza Jumatatu kuwa mlipuko wa hivi karibuni wa homa ya Ebola umeisha nchini humo.
"Mnyororo wa maambukizi umezuiliwa. Kwahiyo natangaza rasmi mwisho wa mlipuko wa 16 wa homa ya Ebola nchini DRC.” Waziri wa Afya wa DRC Roger Kamba ameiambia hafla iliyofanyika mjini Kinshasa.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa DRC Judith Suminwa Tuluka, na maofisa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) na Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC).
Tarehe 4 mwezi Septemba, serikali ya DRC ilithibitisha mlipuko mpya wa homa ya Ebola katika Jimbo la Kasai, ambao ni wa 16 nchini DRC tangu mwaka 1976. Tangu wakati huo, kesi 64 zimeripotiwa Bulape, kanda ya kiafya jimboni Kasai, zikiwemo kesi 53 za wagonjwa waliothibitishwa na 11 za watu walioshukiwa kuambukizwa, huku wengine 43 wakifariki.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



