Lugha Nyingine
Boeing yasema idadi ya abiria wa ndege barani Afrika kuongezeka kwa asilimia 6 kwa mwaka hadi 2044
Kampuni ya kuunda ndege ya Marekani Boeing, imesema Jumanne kuwa idadi ya abiria wa ndege barani Afrika inatarajiwa kuongezeka kwa wastani wa asilimia 6 kwa mwaka hadi itakapofika mwaka 2044, ikichochewa na idadi kubwa ya vijana, kuongezeka kwa kundi la watu wenye kipato cha kati, ukuaji haraka wa miji na uwekezaji unaoendelea katika viwanja vya ndege na muunganisho.
Kwa mujibu wa Mtazamo wa Soko la Biashara la Boeing wa 2025 kwa Afrika, idadi ya ndege za kibiashara za bara hilo inatarajiwa kuongezeka zaidi ya maradufu hadi ndege 1,680 katika kipindi cha miaka 20 ijayo ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya usafiri.
Kampuni hiyo imebainisha kuwa ndege zenye njia moja ya kutenganisha siti pande mbili zitachukua asilimia karibu 70 ya ndege zote mpya zaidi ya 1,200 zitakazokabidhiwa katika kipindi hicho, zikiunga mkono upanuzi wa safari za ndani na safari fupi za kimataifa.
Kampuni hiyo inakadiria uhitaji wa marubani, mafundi na wahudumu wa ndani ya ndege wapya wapatao 74,000 kote barani Afrika katika kipindi hicho cha miaka 20 ijayo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



