Lugha Nyingine
Viongozi wa Afrika na washirika wa maendeleo watoa wito wa kupiga hatua kidijitali ili kukifanyia mageuzi kilimo

Picha hii iliyopigwa Februari 13, 2025 ikionyesha majengo ya Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) huko Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia. (Xinhua/Michael Tewelde)
Maofisa waandamizi wa Umoja wa Afrika (AU) na washirika wa maendeleo wametoa wito wa matumizi mapana na ya dharura ya teknolojia za kidijitali ili kuifanyia mageuzi sekta ya kilimo katika Bara la Afrika.
Wito huo umetolewa Jumatatu wiki hii kwenye hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa kwanza wa AU juu ya Kilimo cha Kidijitali, uliofanyika chini ya kaulimbiu ya “Kuunda Sera ya Kilimo kwa Mustakabali wa Afrika: Uvumbuzi, Matumizi ya Teknolojia za Kisasa Himilivu kwa Tabianchi, na Mageuzi ya Kidijitali kwa Maendeleo Endelevu” uliofanyika katika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia kuanzia jumatatu wiki hii.
Akihutubia mkutano huo, Kamishna wa Kilimo, Maendeleo ya Vijijini, Uchumi wa Bluu na Mazingira Endelevu wa AU Moses Vilakati amesema, kutumia kimkakati teknolojia za kidijitali ni hatua muhimu katika kufikia usalama wa chakula barani Afrika.
Kwa upande wake, mkuu wa Ujumbe wa China katika Umoja wa Afrika Jiang Feng amesema kuongeza kasi ya mafungamano ya kina ya teknolojia za kidijitali na kilimo ni chaguo lisiloepukika na njia muhimu katika kuboresha tija ya kilimo, kuhakikisha usalama wa chakula, na kufikia lengo la kupunguza umaskini vijijini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



