Lugha Nyingine
Juzuu ya 5 ya Kitabu cha Xi Jinping cha "Utawala wa China" yatangazwa Afrika Kusini

Waziri wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa Ikulu ya Afrika Kusini Maropene Ramokgopa akizungumza kwenye shughuli ya kutangaza toleo la Kiingereza la juzuu ya tano ya Kitabu cha Xi Jinping cha "Utawala wa China", mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Desemba 3, 2025. (Xinhua/Chen Wei)
JOHANNESBURG – Shughuli ya kutangaza toleo la Kiingereza la juzuu ya tano ya Kitabu cha Xi Jinping cha "Utawala wa China", imefanyika mjini Johannesburg, Afrika Kusini jana Jumatano ikivutia washiriki wapatao 200, ambapo washiriki hao wamesema kwamba, juzuu hiyo ya tano inaonyesha maendeleo mapya ya Fikra ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Umaalum wa China katika Zama Mpya.
Wamesema kitabu hicho hatua kwa hatua kinaonyesha sifa mahsusi, njia za kivitendo na mafanikio ya ajabu ya njia ya China kujenga mambo ya kisasa, na kinatoa maarifa na mbinu muhimu kwa Nchi za Kusini mwa Dunia zinazofuata kufikia mambo yao ya kisasa.
Wamesema China na Afrika Kusini, zote ni nchi wanachama muhimu wa mfumo wa ushirikiano wa BRICS na nguvu muhimu katika Nchi za Kusini mwa Dunia, zitashirikiana kutekeleza hatua 10 za washirika wa maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa, kuhimiza mapendekezo makubwa manne kwa dunia, na kutoa mchango kwa ajili ya kustawi na kuendeleza Nchi za Kusini mwa Dunia vilevile kutimiza ndoto ya pamoja ya ujenzi wa mambo ya kisasa wa China na Afrika.
Waziri wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa Ikulu ya Afrika Kusini Maropene Ramokgopa amesema kitabu hicho kinajumuisha maeneo muhimu, yakiwemo ya ujenzi wa mambo ya kisasa, mapambano dhidi ya umaskini, ushirikiano wa maendeleo duniani, na uvumbuzi wa kiteknolojia wa China, nk.
"Kinatoa dirisha na hamasa muhimu kwa Nchi za Kusini mwa Dunia kuhusu namna China inavyoelezea na kukabiliana na changamoto duniani," Ramokgopa amesema.
Mwenyekiti wa Baraza la Bunge la Taifa la Afrika Kusini Cedric Frolick amesema kwamba kitabu hicho kinaonyesha kwa pande zote dira ya maendeleo ya siku za baadaye ya China na kinaipa Afrika Kusini dirisha la kutazama maono mapya ya maendeleo na vipaumbele vya sera za nje za China.
"Dhana za kuwaweka watu kwenye kipaumbele cha juu, kutafuta maendeleo ya kijani, kuhimiza ustawi wa pamoja, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja zinatoa maarifa muhimu kwa nchi zinazotafuta kufikia mambo ya kisasa na kuimarisha uwezo wao wa utawala," ameongeza.
Kwenye shughuli hiyo, wageni waheshimiwa wamezawadiwa toleo la Kiingereza la juzuu ya tano ya Kitabu cha Xi Jinping cha "Utawala wa China".
Washiriki pia walibadilishana maoni juu ya kubadilishana uzoefu wa ujenzi wa mambo ya kisasa, uongozi duniani na Nchi za Kusini mwa Dunia, na ushirikiano wa sifa bora wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na mada nyingine.
Shughuli hiyo iliandaliwa kwa pamoja na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China, Kundi la Mawasiliano ya Kimataifa la China, na Ubalozi wa China nchini Afrika Kusini.

Mwenyekiti wa Baraza la Bunge la Taifa la Afrika Kusini Cedric Frolick akizungumza kwenye shughuli ya kutangaza toleo la Kiingereza la juzuu ya tano ya Kitabu cha Xi Jinping cha "Utawala wa China" mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Desemba 3, 2025. (Xinhua/Chen Wei)

Washiriki wakihudhuria shughuli ya kutangaza toleo la Kiingereza la juzuu ya tano ya Kitabu cha Xi Jinping cha "Utawala wa China" mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Desemba 3, 2025. (Xinhua/Chen Wei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



