Kenya yawa mwenyeji wa kongamano la kikanda ili kuchochea mageuzi katika mfumo wa chakula

(CRI Online) Desemba 04, 2025

Maafisa wanaoshiriki kwenye Kongamano la Kujifunza na Majadiliano Barani Afrika wamesema kuwa kuifanyia mageuzi ya mifumo ya chakula ya Afrika ili kuhakikisha inakuwa yenye uwezo wa kuitikia mishtuko ya tabianchi, wadudu, magonjwa, na hali tete ya soko kunahitaji sera zilizoratibiwa na uwekezaji unaozingatia wakulima.

Maafisa hao wamesema hayo jana Jumatano kwenye kongamano hilo linalofanyika kwa siku mbili mjini Nairobi nchini Kenya lililoitishwa na Muungano wa Mamlaka ya Chakula barani Afrika (AFSA) na Shirika la Bioanuwai na Usalama wa Kibiolojia la Kenya.

Kipronoh Ronoh, Katibu Mkuu wa Idara ya Kilimo katika Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo ya Kenya, amesema nchi za Afrika zinahitaji mifumo iliyoratibiwa ya sera ili kuongoza mageuzi katika mifumo ya chakula, kukabiliana na njaa na utapiamlo, na kuongeza mapato ya wakulima.

Kongamano hilo, lililoanza jana Jumatano na limepangwa kumalizika leo Alhamisi, linawakutanisha maafisa waandamizi wa serikali, watafiti na wanaharakati kutoka nchi 16 za Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha