Sudan Kusini yapata dola milioni 52.5 za Marekani ili kuongeza uhimilivu kwenye maeneo yenye udhaifu wa kuathiriwa na mafuriko

(CRI Online) Desemba 04, 2025

Sudan Kusini imesema imepata jumla ya dola milioni 52.5 za Marekani za ufadhili wa tabianchi ili kuongeza uhimilivu kwenye maeneo yenye udhaifu wa athari za mafuriko ya mara kwa mara.

Waziri wa Mazingira na Misitu wa Sudan Kusini Mabior Garang Mabior amesema jana Jumatano kwamba pesa hizo zinajumuisha dola milioni 50 kutoka Mfuko wa Kijani wa Tabianchi (GCF) na dola nyingine milioni 2.5 za ufadhili wa pamoja kutoka kwa washirika wengine.

"Mradi huo unaweka msisitizo maalum kwa jamii zilizolazimika kukimbia makazi yao na zile zinazowapokea, ukihakikisha masuluhisho jumuishi ya kuhimili hali ambayo hayamwachi mtu yeyote nyuma." Garang amesema.

Mpango huo, ambao utaanza mwanzoni mwa mwaka 2026, utajikita katika majimbo ya Kaskazini ya Bahr el Ghazal na Warrap kwa kufungamanisha usimamizi wa maji, kilimo endelevu, na usimamizi wa hatari za maafa, huku ukijikita mahsusi kwa jamii zilizolazimika kukimbia makazi yao na zile zinazowapokea.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha