UN yatenga dola za kimarekani milioni 6 kwa watu waliolazimika kukimbia makazi yao nchini Msumbiji

(CRI Online) Desemba 04, 2025

Umoja wa Mataifa umetenga dola za kimarekani milioni 6 jana Jumatano kwa ajili ya watu waliolazimika kukimbia makazi yao kutokana na vurugu kaskazini mwa Msumbiji, Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Kibinadamu na Kuratibu Misaada ya Dharura Tom Fletcher ameruhusu msaada huo kutoka kwenye Mfuko Mkuu wa Mwitikio wa Dharura (CERF) ili kuongeza juhudi za uungaji mkono wa kuokoa maisha kwa watu 120,000 waliokimbia makazi yao jimboni Nampula.

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa limesema, hadi kufikia Jumanne wiki hii, watu karibu 100,000 kati yao walikuwa wamekimbia makazi yao tangu mwezi Novemba wakati mapigano yaliposambaa jimboni humo.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha