Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron awasili Beijing kwa ziara ya kitaifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 04, 2025

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa akiwasili Beijing, mji mkuu wa China, Desemba 3, 2025. (Xinhua/Cai Yang)

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa akiwasili Beijing, mji mkuu wa China, Desemba 3, 2025. (Xinhua/Cai Yang)

BEIJING - Kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping wa China, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amewasili Beijing, mji mkuu wa China jana Jumatano kwa ziara ya kitaifa nchini China ambayo imepangwa kuendelea hadi kesho Ijumaa.

Hii ni mara ya nne kwa ya Rais Macron kufanya ziara ya kiserikali nchini China na ni ziara yake kufuatia ziara ya kihistoria ya kitaifa ya Rais Xi nchini Ufaransa mwaka jana ambayo iliadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Ufaransa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema wakati wa ziara hiyo, Rais Xi atafanya mazungumzo na Macron ili kuongoza kwa pamoja maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ufaransa chini ya hali mpya. Aidha, marais hao wawili pia watabadilishana maoni kwa kina juu ya masuala nyeti ya kimataifa na ya kikanda.

“China inapenda kushirikiana na Ufaransa kuchukua ziara hii kama fursa ya kutetea moyo wa kuongoza kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Ufaransa, kuimarisha mawasiliano ya kimkakati, kuzidisha ushirikiano wa kivitendo, na kufanya kazi kwa ajili ya uratibu wa karibu zaidi katika masuala ya pande nyingi,” msemaji wa wizara hiyo amesema.

Ameongeza kuwa, pande hizo mbili zinaweza kupiga hatua mpya katika ushirikiano wao wa kimkakati wa pande zote, kuhimiza maendeleo mazuri na tulivu ya uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya, na kutoa mchango mkubwa zaidi katika ushirikiano wa pande nyingi na dunia yenye amani, utulivu na ustawi.

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa akikaribishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), alipowasili Beijing, mji mkuu wa China, Desemba 3, 2025. (Xinhua/Cai Yang)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha