Msumbiji na China zadumisha ushirikiano wa karibu katika kuunga mkono watu wenye ulemavu

(CRI Online) Desemba 05, 2025

Gavana wa Jimbo la Maputo la Msumbiji Manuel Tule amesema Msumbiji na China zinafurahia jadi ya muda mrefu ya urafiki na historia ya kuungana mkono katika kusaidia watu wenye ulemavu.

Bw. Tule amesema hayo Jumatano kwenye hafla iliyofanyika katika Wilaya ya Moamba kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu.

Katika hafla hiyo, Ubalozi wa China nchini Msumbiji umechangia viti vya magurudumu, vifaa vya usaidizi, vitu vya mahitaji ya kila siku pamoja na chakula, vyenye thamani ya dola elfu 28 za Kimarekani, kwa wenyeji wenye ulemavu.

Akizungumzia msaada huo, Bw. Tule amesema mchango huo utaboresha maisha ya watu wenye ulemavu, na kwamba ushirikiano wa pande mbili katika nyanja hiyo utaendelea kunufaisha watu wa nchi hizo mbili.

Akihutubia kwenye hafla hiyo, Balozi wa China nchini Msumbiji Zheng Xuan amesema kuwa China na Msumbiji zina malengo ya pamoja katika kulinda haki za watu wenye ulemavu na kuwawezesha kuwa washiriki, wachangiaji na wanufaika wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha