Maafisa na wataalamu watoa wito wa ushirikiano zaidi kati ya China na Afrika katika maendeleo ya rasilimali watu

(CRI Online) Desemba 05, 2025

Maafisa na wataalamu wametoa wito wa kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya China na Afrika katika maendeleo ya rasilimali watu, huku wakipongeza ujengaji uwezo na uchangiaji uzoefu wa China wa mara kwa mara.

Wito huo umetolewa Jumatano wiki hii kwenye hafla ya kusherehekea ushirikiano kati ya China na Afrika katika maendeleo ya rasilimali watu iliyofanyika katika makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Mkuu wa Ujumbe wa China katika AU, Jiang Feng, alizungumzia matokeo ya ushirikiano wa manufaa kwa pande zote kati ya China na Afrika katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya rasilimali watu, uhusiano wa kijamii na kiuchumi, shughuli za kubadilishana utamaduni, na uhusiano wa kati ya watu.

Kamishna wa AU anayeshughulikia Kilimo, Maendeleo Vijijini, Uchumi wa Bluu, na Mazingira Endelevu Moses Vilakati, amepongeza "uungaji mkono na ushirikiano usioyumba" wa China kwa Afrika.

Hafla hiyo iliwaleta pamoja wanadiplomasia wa China na Afrika, maafisa waandamizi wa AU, na wawakilishi wa wataalamu wa Afrika ambao ni wanufaika wa mipango ya mafunzo inayofadhiliwa na China.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha