Lugha Nyingine
Vurugu zinazoongezeka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati zawatia wasiwasi watoa misaada ya kibinadamu
Watoa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa walisema Alhamisi kwamba wana wasiwasi juu ya athari za vurugu za kutumia silaha kwa raia wa kusini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ilinukuu vyanzo vya ndani vinavyoripoti mashambulizi katika eneo la Mboki Jumapili na Jumatatu, ambayo yalisababisha mauaji ya raia kadhaa na kuongeza mvutano kati ya jamii. Nyumba kadhaa zilichomwa moto, na vurugu hizo zilifanya watu wapatao 1,000 kukimbia makazi yao, ambao waliripotiwa kutafuta usalama katika kanisa la Katoliki la eneo hilo.
OCHA ilibainisha kuwa Mboki imeshuhudia mapigano ya mara kwa mara, huku ufikiaji wa misaada ya kibinadamu ukiwa mgumu sana kutokana na ukosefu wa usalama na mawasiliano duni ya simu.
OCHA ilifafanua kuwa ingawa hali imeboreka katika baadhi ya maeneo ya CAR, vurugu zinaendelea kuongeza mahitaji katika maeneo mengine ambapo watu 50,000 wanahitaji msaada wa kibinadamu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



