Semina ya haki za binadamu ya China na Afrika Kusini yafanyika Pretoria

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 05, 2025

Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Haki za Binadamu wa China Li Hongkui akizungumza kwenye Semina ya Haki za Binadamu ya China na Afrika Kusini 2025 mjini Pretoria, Afrika Kusini, Desemba 4, 2025. (Xinhua/Chen Wei)

Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Haki za Binadamu wa China Li Hongkui akizungumza kwenye Semina ya Haki za Binadamu ya China na Afrika Kusini 2025 mjini Pretoria, Afrika Kusini, Desemba 4, 2025. (Xinhua/Chen Wei)

PRETORIA, Afrika Kusini - Semina ya Haki za Binadamu ya China na Afrika Kusini 2025 chini ya kaulimbiu ya "Mfumo wa pande nyingi na Utambuzi wa Haki ya Maendeleo," imefanyika jana Alhamisi mjini Pretoria, mji mkuu wa kiutawala wa Afrika Kusini ambapo shughuli hiyo ilikutanisha wajumbe wapatao 50 kutoka nchi zote mbili.

Wajumbe katika semina hiyo walijadili mada, zikiwemo za mapendekezo manne makubwa duniani yaliyopendekezwa na China na usimamizi wa haki za binadamu duniani, na ushirikiano wa kivitendo kati ya China na Afrika Kusini na kusukuma mbele haki ya maendeleo.

Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Haki za Binadamu wa China Li Hongkui amesema kuwa, mambo ya haki za binadamu duniani yanakumbwa na changamoto kubwa, na amehimiza pande mbalimbali kufanya juhudi kuimarisha mawasiliano, kupata maafikiano makubwa zaidi juu ya maendeleo ya haki za binadamu miongoni mwa Nchi za Kusini, na kwa pamoja kulinda ushirikiano wa kweli wa pande nyingi.

Li pia ametoa wito wa kuhimiza ushirikiano wa sifa bora wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ili kuziba pengo la maendeleo kati ya Nchi za Kusini na za Kaskazini, vilevile kuhakikisha kwamba maendeleo yananufaisha nchi zote.

David Monyae, mkurugenzi wa Kituo cha Masomo ya Afrika na China katika Chuo Kikuu cha Johannesburg, amesema kwamba kusambaratika kwa mfumo wa pande nyingi katika miaka ya hivi karibuni kumepunguza kwa kiasi kikubwa haki ya maendeleo, hasa ya watu wa Nchi za Kusini.

Akipongeza semina hiyo kufanyika kwa wakati unaofaa, amesisitiza kwamba haki ya maendeleo lazima ijengwe katika hali halisi, utamaduni na uzoefu wa kihistoria za kila nchi, na kwamba hakuna nchi yenye mamlaka ya kuweka viwango vyake kwa wengine.

Wajumbe wanasema kuwa, China na Afrika Kusini zina maafikiano mapana katika kutetea mfumo wa pande nyingi na kuhimiza kujiendeleza kwa pamoja.

Wamesema nchi zote mbili, zikiwa wanachama muhimu wa Nchi za Kusini wenye mitazamo inayofanana juu ya haki za binadamu, zinapaswa kuimarisha mawasiliano na kufunzana katika usimamizi wa haki za binadamu, kutekeleza kwa pamoja mapendekezo manne makubwa duniani, na kutoa mchango katika kujenga usimamizi wa haki za binadamu duniani ulio wa haki na usawa zaidi.

Shughuli hiyo iliandaliwa kwa pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Haki za Binadamu wa China na Kituo cha Masomo ya Afrika na China katika Chuo Kikuu cha Johannesburg. 

Wajumbe wakiwa kwenye Semina ya Haki za Binadamu ya China na Afrika Kusini 2025 mjini Pretoria, Afrika Kusini, Desemba 4, 2025. (Xinhua/Chen Wei)

Wajumbe wakiwa kwenye Semina ya Haki za Binadamu ya China na Afrika Kusini 2025 mjini Pretoria, Afrika Kusini, Desemba 4, 2025. (Xinhua/Chen Wei)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha