China yaitaka Japan kuacha mara moja hatua hatari za kusumbua mazoezi na mafunzo ya kawaida ya kijeshi ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 08, 2025

BEIJING - China inaitaka Japan kuacha mara moja hatua zake hatari za kusumbua mazoezi na mafunzo ya kawaida ya kijeshi, na kuacha taarifa zote potoshi zisizowajibika na ulaghai wa kisiasa, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema.

Msemaji huyo ameyasema hayo wakati akijibu swali kuhusu kauli zilizotolewa na Waziri wa Ulinzi wa Japan Shinjiro Koizumi kwenye mkutano wa dharura na waandishi wa habari mapema asubuhi jana Jumapili, Desemba 7.

Msemaji huyo amesema kwamba Jeshi la China limeshaeleza msimamo wake makini juu ya suala hilo na ukweli wa mambo uko dhahiri kabisa kwamba ni upelelezi wa karibu na usumbufu wa mara kwa mara uliofanywa na ndege za kivita za Japan dhidi ya shughuli za kawaida za kijeshi za China ambazo zimesababisha hatari kubwa zaidi kwa usalama wa baharini na angani.

"China haikubali kile kinachoitwa malalamiko kutoka Japan na imekataa papo hapo na kutoa malalamiko ya kupinga hatua hiyo kwa Japan huko Beijing na Tokyo" ameongeza.

Msemaji huyo amesema, chini ya hali ya sasa, Japan, kwa maksudi inapandisha kwa chuki suala linaloitwa la "mwangaza wa rada", inatoa shutuma za uongo dhidi ya China ili kuchochea mvutano na kupotosha jumuiya ya kimataifa. Amesema, huu ni uovu mtupu, na China inapinga vikali kitendo hicho.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha