Lugha Nyingine
Watoto 50 wafariki nchini Somalia kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa diphtheria
Wizara ya Afya na Huduma za Kibinadamu ya nchini Somalia imethibitisha kuwa, mlipuko mpya wa ugonjwa wa diphtheria umesababisha vifo vya watoto 50 na kuambukiza wengine zaidi ya 1,000 nchini humo.
Katika taarifa yake iliyotolewa jana Jumapili, Wizara hiyo imesema watoto wenye umri wa miaka kati ya mitano hadi 15 ndiyo wameathirika zaidi na ugonjwa huo.
Katika kukabiliana na mlipuko huo, Wizara hiyo imezindua kampeni za chanjo ili kudhibiti ugonjwa huo, na kwamba kampeni hiyo itaanza Desemba 15 na itaendelea kwa siku tano.
Wizara hiyo imesema, watoto wote popote walipo, vijijini, hospitalini, na shuleni watapewa chanjo hiyo, na imetoa wito kwa wazazi kupeleka watoto wao katika vituo vilivyotengwa ili kusaidia kudhibiti kile ilichokielezea kuwa ni ugonjwa unaoua.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



