Lugha Nyingine
Idadi ya vifo katika shambulizi la droni nchini Sudan yafikia 114
Serikali ya Jimbo la Kordofan Kusini nchini Sudan imesema, idadi ya vifo kutokana na shambulizi la droni lililotokea Alhamisi wiki iliyopita huko Kalogi, katika jimbo hilo imefikia 114.
Gavana wa jimbo hilo Mohamed Ibrahim Abdel Karim amesema katika taarifa jana Jumapili kuwa, huenda idadi hiyo ya vifo ikaongezeka kwani baadhi ya watu waliojeruhiwa vibaya wamehamishiwa hospitalini nje ya Kalogi kutokana na huduma chache za matibabu za jimbo hilo.
Mamlaka za Serikali ya Sudan zimelishutumu kundi la upinzani la SPLM tawi la Kaskazini linaloongozwa na Abdelaziz Al-Hilu, kwa kushirikiana na wanamgambo wa Vikosi vya Uungaji Mkono wa Haraka (RSF) kufanya shambulizi hilo ambalo lililenga eneo la raia.
Hadi sasa RSF na SPLM-N bado hazijatoa tamko lolote kufuatia shambulizi hilo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



