Video: Ni hisia nzuri kiasi gani kusoma kwenye chumba kinachotazamana na bahari?

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 08, 2025

Eneo la Majaribio ya Uvumbuzi wa Elimu ya Kimataifa la Hainan Lingshui Li'an lililojengwa kwa pamoja na Wizara ya Elimu ya China na Serikali ya Mkoa wa Hainan, ni eneo pekee katika Bandari ya Biashara Huria ya Hainan lenye dhamira ya kufungua mlango katika sekta ya elimu.

Maktaba inayokutazamana na bahari ni jengo kinara ndani ya eneo hilo, na udhihirisho dhahiri wa mbinu yake ya kiuvumbuzi ya "kuchangiana kwa majengo makubwa + vyuo vidogo", inayomaanisha matumizi ya kuchangia majengo ya umma, na vyuo mahsusi vidogo kwa kila chuo kikuu.

Kwa sasa vyuo vikuu 26 vimeshasaini makubaliano kuanzisha shughuli zao kwenye eneo hilo, vikiwa na idadi ya jumla ya wanafunzi zaidi ya 1,000 wa kimataifa. Falsafa za uvumbuzi wa elimu zitahimiza mfumo wa vipaji wenye kufungua mlango zaidi kwa ajili ya ujenzi wa Bandari ya Biashara Huria ya Hainan.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha