Lugha Nyingine
Uzuri wa Majira: Theluji Kubwa
Habari zenu nyote. Mimi ni Sisi, mpenda kutalii! Leo ni Daxue, au Theluji Kubwa, kipindi cha tatu cha majira ya baridi katika kalenda ya kilimo ya China. Kinaashiria kuingia kwenye kipindi cha katikati ya majira ya baridi wakati ambapo hali ya hewa inabadilika kuwa baridi kali. Sasa, nimesimama juu ya Milima Changbai, ambayo ni mlima cha juu zaidi zaidi kaskazini mashariki mwa China. Ninapoyatazama, mandhari ya theluji kwenye Ziwa Tianchi ni safi na ang’avu, na viwanja vya kuteleza kwenye theluji pia zimefunguliwa kikamilifu. Njoo ufungue siri za asili na hekima ya maisha ya kipindi cha Daxue katika mandhari hizi za baridi zinazojaa theluji!
Je, wajua? Kipindi hiki cha "Daxue" hakihusiani moja kwa moja na kuanguka theluji nyingi katika utabiri wa hali ya hewa; badala yake, kinaonyesha sifa za hali ya hewa katika kipindi hiki. Kipindi cha Daxue kinapowasili, wanaotamani zaidi kuona theluji ni wakulima. Tangu zama za kale, theluji imekuwa ishara ya mavuno mazuri. Kama msemo usemavyo, "Theluji ya wakati unaofaa inaashiria mavuno mazuri." Hii ni hekima ya kilimo iliyorithiwa kutoka kwa mababu zetu. Theluji nene hufunika mazao yanayokua wakati wa majira ya baridi kama blanketi, ikiyalinda dhidi ya baridi kali na kurutubisha udongo inapoyeyuka mwaka unaofuata. Siku hizi, mashamba mengi yanatumia vihisio vya maalumu vya kufuatilia theluji ili kudhibiti kisayansi mazingira ya ukuaji wa mazao. Hivyo hekima ya jadi ya kilimo inaunganishwa na teknolojia ya kisasa ili kusaidia kuhakikisha mavuno mengi.
Kwa upande wa chakula, kanuni muhimu wakati wa Daxue ni rahisi: "ukijilisha vyema wakati wa Daxue, hutateseka kwa baridi mwaka mzima." Kusini mwa China, watu huchovya na kuhifadhi nyama, wakati huohuo kaskazini mwa China, watu hunywa supu ya kondoo na uji wa viazi vitamu ili kupambana na baridi. Mila zote mbili zinafaa kikamilifu kwa msimu.
Hekima na furaha ya Daxue haipo China pekee! Nchi nyingi pia zinaandaa matamasha yao ya theluji, kama vile shughuli za kitamaduni katika Kijiji cha Santa Claus huko Rovaniemi, Finland; na Tamasha la Kuteleza kwenye Theluji la Holmenkollen huko Oslo, Norway. Ingawa desturi hutofautiana, moyo wa kukumbatia hali ya majira na kufurahia majira ya baridi ni wa pamoja, na huleta msisimko wa kitamaduni unaovuka mipaka.
Nikiwa nimesimama hapa chini ya Milima Changbai, theluji ikisagika chini ya miguu yangu na kushikilia bakuli la moto la supu ya kuku ya ginseng mikononi mwangu, nikiangalia watalii wakipita, ndipo ninaelewa maana ya kina zaidi ya "Theluji kubwa ilipoisha, jua likianza kuonekana, bado siwezi kujizuia kupanda jengo refu mara kwa mara ili kufurahia maandhari." Je, kwenu kumeanza kuanguka theluji? Karibu usimulie hali ya kipindi cha Daxue kutoka nyumbani kwenu!
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



