Kikosi cha polisi wapanda farasi cha "Gyrfalcon" chalinda mbuga katika mpaka wa kaskazini wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 05, 2025
Kikosi cha polisi wapanda farasi cha
Picha iliyopigwa Desemba 2, 2025 ikionyesha kikosi cha polisi wapanda farasi cha "Gyrfalcon" wakifanya doria kwenye Mbuga ya Chenbarhu Banner iliyofunikwa na theluji huko Hulun Buir, Mkoa wa Unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China. (Xinhua/Ma Jinrui)

Ndani kabisa kwenye mbuga iliyofunikwa na theluji huko Chenbarhu Banner, Mkoa wa Unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China, kikosi cha polisi wapanda farasi kikifanya doria kinakabiliwa na upepo mkali na theluji. Wanafanya doria za ulinzi wa usalama na kufanya usimamizi kwenye mbuga kubwa katika eneo lenye kilomita za mraba 18,600.

Wakiwa na farasi waliofunzwa vizuri, ambao kila mmoja wao amepitia mafunzo ya hatua kwa hatua kwa zaidi ya miezi sita, kikosi hicho cha polisi ni kama "ishara ya usalama" kwenye mbuga hiyo, wakilinda wafugaji mifugo wenyeji kwa mwaka mzima.

Kikosi hicho cha polisi wa farasi ya "Gyrfalcon", ambacho kilianzishwa mwaka wa 2015, ni cha kwanza cha aina yake huko Hulun Buir.

Katika muongo mmoja uliopita, maofisa wa polisi wa kikosi hicho wamekuwa wakijitolea katika kazi zao chini ya hali ngumu kwenye mpaka wa kaskazini wa China. Iwe ni kuvumilia miale mikali ya urujuanimno wakati wa majira ya joto au kufanya mafunzo maalum kwenye viwanja vya theluji vyenye halijoto inayofikia nyuzi joto 40 chini ya sifuri wakati wa majira ya baridi, kikosi hicho hakijawahi kusitisha kutekeleza majukumu yake siku zote.

Mbali na doria na mafunzo ya mara kwa mara, kikosi hicho pia kimechangia katika usalama wa shule za mitaa, ikiongoza magari na kusindikiza wanafunzi kupita mitaa iliyofunikwa na theluji.

Hadi sasa, jumla ya umbali wa doria wa kikosi hicho umezidi kilomita 140,000 na kimesaidia wakazi karibu 700 kuepuka hatari. Kutoka kwenye mbuga hadi miji ya karibu, kikosi hicho cha polisi wapanda farasi cha "Gyrfalcon" ni mlinzi mwaminifu wa watu wa huko na ardhi ya eneo hilo.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha