Uongozi wa CPC wafanya mkutano kuhusu kazi ya uchumi mwaka 2026 na vifungu vya kazi ya utawala wa nchi kwa mujibu wa sheria

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 09, 2025

BEIJING - Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) jana Jumatatu ilifanya mkutano wa kuchambua na kujadili kwa makini kazi ya uchumi ya mwaka 2026 na kupitia vifungu vya kazi ya uongozi wa CPC kuhusu utawala wa nchi kwa mujibu wa sheria katika mambo yote. Mkutano huo uliongozwa na Xi Jinping, katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC.

Mkutano huo ukieleza kuwa mwaka huu ni mwaka wenye umuhimu katika mchakato wa kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa wa China, umesema China imetekeleza sera za jumla za kuhimiza juhudi zaidi za kupata mafanikio, na malengo makuu ya maendeleo ya uchumi na jamii yatatimizwa kwa mafanikio.

"Katika miaka mitano iliyopita, China imekabiliana na changamoto mbalimbali, ambapo nguvu za uchumi, sayansi na teknolojia, na ulinzi wa taifa, vilevile nguvu za mambo ya utamaduni, mfumo na utaratibu na diplomasia zimeongezwa na kuimarishwa kwa udhahiri" mkutano huo umesema.

Mkutano huo umesisitiza kwamba ili kufanya vizuri kazi za uchumi mwaka ujao, ni muhimu kutekeleza kikamilifu na kwa makini mawazo mapya ya maendeleo katika sekta zote, kuanzisha haraka muundo mpya wa maendeleo, kuhimiza maendeleo ya sifa bora ya juu, kushikilia kanuni ya jumla ya kutafuta maendeleo wakati wa kuhakikisha usalama, na kuratibu vizuri kazi za uchumi za ndani na juhudi katika mambo ya uchumi na biashara ya kimataifa.

Mkutano huo pia umedhihirisha kuwa ni muhimu kufanya mpango wa jumla wa maendeleo na usalama, kutekeleza sera za jumla za kuhimiza juhudi zaidi za kupata ufanisi, kuzifanya sera kuwa zenye upeo wa kutazama mbele, za kulenga hali halisi, na za kutoa nguvu za pamoja katika kazi zote, kuendelea kupanua mahitaji ya ndani na kuboresha utoaji wa bidhaa, kukuza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora kulingana na hali halisi za sehemu husika, kujitahidi kuendeleza soko la pamoja la nchi nzima, kuendelea kuzuia na kupunguza hatari katika maeneo muhimu, na kujitahidi kutuliza hali ya ajira, shughuli za kampuni na viwanda, masoko na matarajio ili kuhakikisha mwanzo mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa 15 wa Maendeleo ya Miaka Mitano (2026-2030).

"Ni lazima kudumisha jukumu ongozi la mahitaji ya ndani, kufuata mbinu za kujipatia maendeleo kwa kutegemea uvumbuzi, na kuhimiza kazi muhimu za mageuzi," mkutano huo umeeleza.

Mkutano huo umesisitiza pia kuwa, ni lazima kuongeza imani katika kufuata njia ya utekelezaji wa sheria wa ujamaa wenye umaalum wa China, na kusukuma mbele usimamizi wa kazi za pande zote mbalimbali kwa mujibu wa sheria.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha