Lugha Nyingine
Kuunga mkono "Taiwan ijitenge" kunakiuka katiba ya China na sheria za kimataifa: Wang Yi

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Johann Wadephul mjini Beijing, mji mkuu wa China, Desemba 8, 2025. (Xinhua/Dai Tianfang)
BEIJING - Jaribio la kutaka "Taiwan ijitenge" linamaanisha kugawanya ardhi ya China, na kuunga mkono "Taiwan Ijitenge" ni sawa na kuingilia kati mambo ya ndani ya China, ambayo ni kukiuka katiba ya China na sheria za kimataifa, amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi mjini Beijing jana Jumatatu alipofanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Johann Wadephul, ambapo Wang amefafanua kuhusu hali halisi ya kihistoria na msingi wa kisheria kuhusu suala la Taiwan.
"Taiwan imekuwa sehemu ya China tangu enzi za kale," Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China amesema, akiongeza kuwa Azimio la Cairo lililotolewa mwaka 1943 lilisema kidhahiri kwamba maeneo yote ambayo Japan ilikuwa imeyaiba kutoka China, kama vile Taiwan, yanapaswa kurejeshwa kwa China.
"Kifungu cha 8 cha Tangazo la Potsdam lililotolewa kwa pamoja na China, Marekani, Uingereza na Umoja wa Kisovieti mwaka 1945 kilieleza kwamba Azimio la Cairo litatekelezwa." Wang amesisitiza.
Amesema Agosti 15, 1945, Japan ilijisalimisha bila masharti, huku Mfalme wa Japan akiahidi kutekeleza kwa uaminifu Tangazo la Potsdam. Ameongeza kuwa, Oktoba 25, 1945, serikali ya China ilitangaza kurejesha utekelezaji wa mamlaka na ukamilifu wa ardhi ya China juu ya Taiwan, na hafla ya kupokea kujisalimisha kwa Japan katika Mkoa wa Taiwan wa uwangja wa vita wa China la nchi washirika ilifanyika Taipei.
Ameeleza kwamba, mwaka 1949, Jamhuri ya Watu wa China (PRC) ilichukua nafasi ya Jamhuri ya China, na Serikali Kuu ya Watu wa China ikawa serikali pekee halali ya China nzima." Kwa matokeo ya kawaida, serikali ya PRC inapaswa kuwa na kutekeleza mamlaka juu ya eneo lake lote, ikiwa ni pamoja na Taiwan" ameongeza.
Amesema kwamba katika mkutano wake wa 26 Oktoba 1971, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio 2758, ambalo liliahidi kurejesha haki zake zote kwa PRC, na kuwafukuza mara moja "wawakilishi" wa utawala wa Taiwan kutoka mahali pa Umoja wa Mataifa. Amesema, maoni rasmi ya kisheria ya Umoja wa Mataifa yanathibitisha kwamba Taiwan ni mkoa wa China.
Taarifa ya Pamoja kati ya China na Japan ya 1972 inasema kwamba "Serikali ya Japan inatambua Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kuwa Serikali pekee halali ya China. Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China inasisitiza kwamba Taiwan ni sehemu isiyotengeka ya ardhi ya Jamhuri ya Watu wa China. Serikali ya Japan inaelewa kikamilifu na kuheshimu msimamo huu wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, na inadumisha bila kuyumba msimamo wake chini ya Kifungu cha 8 cha Tangazo la Potsdam."
Amesema Mkataba wa Amani na Urafiki wa 1978 Kati ya China na Japan unathibitisha kwamba kanuni zilizowekwa kwenye Taarifa ya Pamoja kati ya China na Japan zinapaswa kuzingatiwa kwa makini.
"Hadhi ya Taiwan kama ardhi ya China imethibitishwa bila shaka yoyote na bila kubadilika na mfululizo wa uhalisia wa mambo wa kihistoria na kisheria," amesema Wang.
"Kiongozi wa sasa wa Japan hivi karibuni alitoa kauli zisizo na uwajibikaji kuhusu Taiwan," amebainisha Wang, akieleza kwamba hii inakiuka vibaya mamlaka na ukamilifu wa ardhi ya China, inakiuka waziwazi ahadi ambazo Japan imetoa kwa China, inapinga moja kwa moja matokeo ya ushindi katika Vita vya Pili vya Dunia na utaratibu wa kimataifa wa baada ya vita, na inahatarisha kwa kiasi kikubwa amani ya Asia na duniani kwa ujumla.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China(CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Johann Wadephul mjini Beijing, mji mkuu wa China, Desemba 8, 2025. (Xinhua/Dai Tianfang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



